GET /api/v0.1/hansard/entries/383778/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 383778,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/383778/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ya ardhi, basi Wakenya wanapata tumbo joto kwa sababu ardhi ndio imeletea misukosuko katika nchi hii. Kama tunataka kuhakikisha kuwa Wakenya wanaishi maisha bora kama ulikuwa na kiosk, urudishiwe kiosk . Kama ni nyumba upewe nyumba, basi tutakuwa tunasema tuangalie Wakenya wawe na haki, wawe na nyumba nzuri na makao mazuri. Lakini tunapozungumza jambo la Internally Displaced Persons (IDPs) tunazungumza habari ya mashamba na hiyo ndio inapingwa. Unaona inapingwa kwamba wanaotolewa kutoka mahali pengine wakiletwa kaunti nyingine basi watu wa pale wanapinga kwa sababu tunaangalia mashamba. Kwa hivyo, nataka nitoe tofauti kwamba waliofurushwa makwao basi warudishwe. Kwa mfano, tunasema watu walioelewana na kuna maelewano na kama ulikuwa na shamba ekari hamsini limechukuliwa na nani, si liko mahali lilikuwa? Kwa hivyo rudi pale pale na Serikali itakupa usalama. Kwa hivyo, tukiangalia mambo haya tuwaulize kwa nini walifurushwa. Tusiangalie ya siasa peke yake, tuangalie ya zama maanake tulianza pale. Tulianza kupotea barabara miaka ya zamani. Sasa tunazidi kupotea. Tuangalie tulipotelea wapi, tupate ramani, turekebishe na Kenya iwe na amani. Makusudio yangu ni kwamba kila kaunti ingeangalia maslahi ya waliofurushwa katika makaazi yao ili kuwe na makaratasi, historia na hesabu kamili. Vile sasa tuko na Serikali mbili, Serikali ya Kitaifa na Serikali ya majimbo, Serikali ya majimbo, kwa mfano Taita Taveta County kuna watu 10,000, basi ichukue jukumu hilo ikishirikiana na Serikali ya Kitaifa ili wale 10,000 watendewe haki, iwe ni mashamba ama ili wapate haki waishi katika hali ya heshima. Lakini tukianza kusema kwamba tunatoa watu kutoka kona ya ng’ambo ile na kuwapeleka kule kwingine, tumeona Wakenya wakikataa. Tutaongeza chuki na ukabila. Kwa hivyo, katika madhumuni yangu, kwa mfano, jana nilikuwa mjini nikaona vijana wanakimbizana wakisema wametolewa kwa boma ambalo wamekaa zaidi ya miaka ishirini. Hiyo ni kufurushwa kutoka makaazi yao. Si lazima iwe ni miaka mingi. Hata jana walifurushwa na wamekaa pale kwa miaka zaidi 25. Kwa hivyo, kama tunataka tutatue tatizo kama la jana basi tufikirie tutawapatia nini ili waendelee kupata riziki. Lakini tukisema kwamba vile walifurushwa ni lazima wapewe shamba basi swala hilo litakuwa ngumu kulitatua. Tulitatue kulingana na shida ya mtu. Nimekuwa Bunge tangu mwaka 2008, pesa zilirundikwa nyingi mwaka 2009. Tukiangalia ile ripoti iliyotolewa na Waziri aliyekuwa wa Mipango Maalum na Maendeleo, watu wale ambao walikuwepo walipewa mashamba - Walioko sasa ni watu wanachukulia uhamishaji kama biashara. It is now being commercialized. Ndio unaona watu wanatoka wapya wanaenda kujiandikisha kwa maana wanajua Serikali itawapatia pesa na mashamba. Ndio maana nikasema kwamba kila kaunti ipewe jukumu la kuangalia watu wao kwa sababu wanajuana. Leo nikija hapa nimetoka kwangu na kabla sijapigiwa kura, niko na kwetu. Mambo yakiwa moto Nairobi nitarudi kwetu. Kila mtu ana mahali alitoka kwa hivyo arudi pale na akirudi pale kama hana makao atatengenezewa makao na watu wa pale. Tukifanya hivyo, basi, tutatatua swala la mashamba. Kama IDP ni mashamba basi mkisema mnawaleta kwetu watu wataandamana. Kwa mfano kama wale vijana wa Grogan, kama mtu alikuwa na kioski basi apewe kioski mahali pengine na hiyo tutakuwa tumemsaidia kustawi. Lakini kama itakuwa kwamba alitolewa Grogan na alikuwa na kioski na tunampeleka kwengine apewe The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}