GET /api/v0.1/hansard/entries/383780/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 383780,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/383780/?format=api",
"text_counter": 175,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "mashamba ekari mbili, tutakuwa tumekosea. Kwa hivyo ilivyo sasa, haikusema mashamba bali ilisema kwamba Serikali iweke mikakati ili waliofurushwa makwao wapate mahali pa kuishi. Kama ulikuwa na nyumba, kwa nini upewe shamba? Kama ulikuwa na kioski, kwa nini upewe shamba? Tuangalie alikuwa akifanya nini. Kama alikuwa ni fundi wa viatu na akatolewa mahali basi apewe mahali pengine aendelee kushona viatu. Ninafahamu kwamba umrudishie riziki yake ili apate kuendelea na maisha yake ya kawaida. Lakini tunavyozungumzia suala la IDP hapa Kenya, tunalenga mashamba. Tukilenga mashamba, basi, italeta ukabila. Kwa sababu watu wanaona kwamba hawa wanatolewa makwao na kuletwa kwetu kugawanya nchi yetu. Naomba kwamba tuweke utaratibu na kila kaunti ipate hesabu ya watu wao na ipewe jukumu ili iwapatie makao pale. Kama ni pwani basi wapewe mkanda wa kilomita kumi na watu wa pale wakae. Tukisema warudishiwe mashamba yao kutakuwa na vurumai kwa sababu kumejengwa. Kwa hivyo, yafaa wapewe mahali pengine. Pia Serikali ya Kenya ikitaka kupatia watu wake makao ni lazima tubadilishe misingi, tuanze kujenga nyumba ya ghorofa na watu wapewe makao. Si tutakuwa tumewapa nyumba? Kwa hivyo hakutakuwa na haja kumpatia plot kwa sababu amepata makao. Tukifanya hivyo, tutamaliza mambo haya lakini tukisema kwamba IDP lazima wapewe shamba nina hakika tutazungumza mpaka kesho asubuhi. Mashamba yamepungua na ukweli ni kwamba tusibadilishe kwamba IDP ni shamba, tujue kwamba IDP ni watu ambao walifurushwa makwao na tunataka warudishwe walipokuwa. Naunga mkono mabadiliko haya ili tupate historia; bila historia hatuwezi kutibu ya sasa."
}