GET /api/v0.1/hansard/entries/384267/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 384267,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/384267/?format=api",
"text_counter": 120,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo ni ya maana sana. Bi. Spika wa Muda, nimesikiza kwa makini yaliyosemwa na wenzangu. Ningependa kuongezea tu kwamba inahuzunisha sana tunapoangalia mambo yanayotokea katika taifa letu na mambo yanayopewa kipao mbele. Nasema haya kwa sababu Kenya imedhihirisha kwamba inauwezo wa kuwaangalia wananchi wake na kutoa huduma zinazohitajika. Lakini maswala ambayo tunaweka mbele yetu kwa kawaida hayasaidii taifa letu hata kidogo. Nasema haya kwa sababu leo tunajua maswala na masaibu ambayo yametajwa hapa kama viongozi. Tunajua kwamba katika Bajeti mbele ya Bunge sasa ina kitita cha Kshs700 millioni ambazo zitatumika kumnunulia Rais Mstaafu ofisi ya kifahari, aitumie yeye pekee, ilhali tuna mambo haya ambayo tumeyazungumzia hapa. Sisi ni viongozi ambao tunatenda vile tunavyotaka, bila kuwajali waliotuchagua. Hatushughulikii shida za wananchi kwa makini. Ninasema hivi kwa sababu tukitumia Kshs700 millioni kununua ofisi ya Rais Mstaafu, na katika Kaunti 47 hakuna hosipitali, inamaanisha kwamba sisi ni viongozi ambao hatujali. Tukiendelea hivi, hata tukipitisha Hoja hapa za kujenga hosipitali haitakuwa na maana kama hatutakuwa na pesa za kujenga. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}