GET /api/v0.1/hansard/entries/384269/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 384269,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/384269/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi. Spika wa Muda, wauguzi ambao wanatibu watu wetu wanahamia nchi zingine au kufanya maandamano barabarani kila asubuhi wakitaka mishahara mizuri. Yale tunaona ni matumizi ya pesa nyingi kulipia ndege inayotumiwa na mtu mmoja. Tunatumia Kshs25 milioni kwa wakati mmoja kwa safari. Sio sehemu moja ya nchi ambayo ina matatizo, bali ni taifa nzima. Nilikuwa Nyahururu siku ya Ijumaa kuhudhuria mazishi. Yule ambaye nilienda kumzika alipatwa na ugonjwa huko Nyahururu na akaletwa Nairobi. Hii inamaanisha kuwa hakuna hospitali katika sehemu hiyo ambayo ina uwezo wa kumtibu mtu kama huyo. Kwa hivyo, zile hosipitali ambazo zinatajwa kuwa ziko, ni majengo tu ambayo hayana vifaa ndani yake. Bi. Spika wa Muda, katika Kaunti yangu ya Machakos, kuna Hospitali ya Machakos ambayo imepewa nafasi hiyo ya Level 5, lakini haina ambulance. Vile vile, chumba cha kuweka maiti ni kile kilijengwa na mkoloni. Hosipitali hiyo haina jiko na ina zaidi ya vitanda 300. Ukweli ni kwamba ni afadhali kwenda kwa duka kununua tembe kuliko kwenda kwa hiyo hosipitali kutibiwa. Je, hiyo inamaanisha nini? Nakusudia kuleta mabadiliko fulani kwa Hoja hii ya Sen. Machage kusema kwamba hata zile hospitali ambazo ziko ziundwe upya na kupewa vifaa. Hii ni kwa sababu taifa lolote ambalo linataka kujimudu ni lazima lishughulikie mambo matatu, yaani magonjwa, elimu na maji. Haya mambo katika taifa letu hayazingatiwi kamwe. Viongozi wetu ni watu wa kutafuta maisha ya juu. Wanataka mikeka mekundu, magari makubwa, barafu na maua katika ofisi zao. Tukiongea watu wanafikiri kuwa tunafanya siasa. Kule nilikotoka nilihesabu shule kati ya Nakuru na Gilgil na nikajiuliza: Je, tutatumia Kshs53 billioni kuwapatia watoto laptops ilhali nguo zao zimechakaa na kuraruka; madarasa yao yako karibu kuanguka? Tunafaa kupanga kama viongozi na kujua majukumu ambayo tunahitaji kufanya kwa sasa. Lakini tukitaka kuishi kama Wamerekani leo, na huku hatuwezi kupata hata chakula cha kuwapa watu wetu, tutakuwa tunapoteza wakati. Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii."
}