GET /api/v0.1/hansard/entries/384909/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 384909,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/384909/?format=api",
    "text_counter": 136,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Okong’o",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 948,
        "legal_name": "Kennedy Mong'are Okong'o",
        "slug": "kennedy-mongare-okongo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Ningependa kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa na Dkt. Machage, mwenye tajiriba kuu katika udaktari. Janga hii la vijana wetu kutumia madawa ya kulevya ni kubwa sana. Hivi majuzi Rais aliamuru kwamba wale watu wote wanaohusika na biashara ya madawa ya kulevya wanafaa kuchukuliwa hatua kali. Ninamshukuru kwa msimamo wake juu ya madawa haya. Inafaa pia janga hili lichukuliwe kama la kitaifa na liidhinishwe katika sheria ili hatua zichukuliwe za kupambana nalo na kuhusisha watu wote, wakiwemo walimu, viongozi wa kisiasa na dini. Janga hili limeharibu maisha ya vijana wetu. Bw. Naibu Spika, sina mengi kwa sababu nimesikiliza yale yote yaliyosemwa na mhe. Obure alipokuwa akichangia Hoja hii. Ameongea kwa mapana na marefu juu ya janga la madawa ya kulevya. Hivi majuzi tuliona kwenye runinga ekari nyingi za bhangi ambazo zimepandwa katika msitu wa Aberdare. Vijana wengi katika Mkoa wa Pwani hawajielewi kwa sababu wameathirika sana na madawa ya kulevya. Ikiwa janga hili litatangazwa kuwa janga la kitaifa, basi tutapambana nalo kikamilifu. Bw. Naibu Spika, mhe. Lesan amesema kwamba kuna nchi kadhaa ambazo zimeweka mikakati na vikwazo vikali vya kupambana na janga hilli. Kwa mfano, nchi za Uarabuni zimeweka hatua kali dhidi ya kupambana na madawa ya kulevya. Katika nchi zingine adhabu ni kali sana na ndio nilisema kwamba yafaa tuige mfano kama huo ili tuweze kuangalia mambo ya vijana. Pombe ya Kiafrika kama busaa na chang’aa hazikuwa na madhara sana. Hivi majuzi watu ambao wanauza pombe hii wameshikwa na tamaa na kuanza kuweka dawa. Haya madawa yameathiri vijana kote nchini kutoka magharibi, mashariki na kaskazini. Vijana wengi wameathirika sana na pia familia zao zimeathirika. Bw. Naibu Spika, mimi naona kwamba sisi viongozi tuko na jukumu kubwa sana kutoa mchango wetu katika kaunti zetu. Kaunti zetu yafaa ziwe na mipango mwafaka haswa kuhusu jambo hili litakapotangazwa kama jangwa la kitaifa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}