GET /api/v0.1/hansard/entries/384938/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 384938,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/384938/?format=api",
    "text_counter": 165,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chelule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13126,
        "legal_name": "Liza Chelule",
        "slug": "liza-chelule"
    },
    "content": "Asante Sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja iliyoletwa hapa na Seneta (Dkt.) Machage kuhusu madawa ya kulevya na pombe. Ninaposimama hapa, nasimama kama mama; najua wamama wengi sana wameumia kwa sababu watoto wao wamepotea katika mambo ya ulevi na madawa ya kulevya. Ninaposimama, nasimama kwa niaba ya wale wamama walioumia; nasimama pia kwa niaba ya wale wamama waliopoteza mabwana zao; nasimama pia kwa niaba ya wale watoto waliopoteza wazazi wao kwa sababu ya shida ambazo wazazi hao wanapitia. Inatakikana sisi wote tuchukue jukumu hili kama viongozi wa Kenya pamoja na wazazi wote. Bw. Naibu Spika, ningependa kuchukua nafasi hii kusema kwamba kwa wazazi ambao hawana njia ya kutatua shida za watoto wao. Kile kitu kinachotakikana kiangaliwe na Serikali yetu ni kiini cha mambo haya; ni nini inaanzisha mambo haya mpaka inafikia kiwango kwamba watoto wanaamua kuvuta bangi, kunywa pombe na kuishi maisha yaliyozoroteka? Kwa hivyo, ni lazima Serikali ichukue jukumu la kuchunguza kiini cha tatizo hili. Tunajua kwamba kuna watu wengi sana wanaofaidika kutokana na kazi ya kuuza pombe na madawa ya kulevya, na pengine watoto wao hawahusiki katika kuvuta bangi ama kunywa pombe hizo. Inatakikana tuchunguze mahali shida hii inaanzia na kiini cha shida hii kiko wapi. Ningependa kuchukua nafasi hii kuwahimiza na kuwaomba wazazi – mimi nikiwa mmoja wao – tuchunguze na tuchukue jukumu hili pamoja kama wazazi; na Serikali pia ichukue jukumu hili. Bw. Naibu Spika, nimefurahi sana jinsi Serikali imeweza kuchukua jukumu hili. Juzi, watu wawili walishikwa katika uwanja wa Ndege na ilikuwa ni maajabu sana kujua kwamba kumbe watu wanaweza kubeba madawa hayo ya kulevya hata katika miili yao. Naipongeza Serikali kwa sababu iliweza kufanya kazi yake vilivyo. Bw. Naibu Spika, nataka kumuunga mkono Sen. Elachi na wenzangu walioongea kabla yangu, kwa kusema kwamba lazima tuwe na vyuo vinavyoweza kuwasajili watoto wetu baada ya kumaliza kidato cha nne. Lazima tuangalie ni nini watoto wetu watahusika nayo katika maisha yao baada ya shule. Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika, nimesimama kusema yes kwa Hoja hii kwa sababu hii ni shida katika nchi yetu na kama viongozi, yatakikana tuwe tayari kuangalia jinsi tutaweza kuitatua shida hii. Naunga mkono Hoja iliyoletwa hapa na Sen. (Dkt.) Machage. Asante sana, Bw. Naibu Spika."
}