GET /api/v0.1/hansard/entries/384951/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 384951,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/384951/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ningependa kumshukuru Bw. Machage kwa kutuletea Hoja ambayo inanigusa mimi kama mama kutoka Pwani. Waswahili walisema isifuye mvua imenyea. Wakati mvua inaponyesha nyingi, sehemu zingine huwa na mafuriko. Mafuriko ya mihadarati yamekuwa swala sugu sana. Kitu ambacho kinachonishangaza ni kwamba kuna wakati tuliposikia kuhusu Artur Margaryan. Kuna wakati akina mama wa Mombasa waliandamana na hata tukasema tutavua nguo ili tupatiwe majina ya walanguzi wa madawa ya kulevya. Watu hao walitajwa na mpaka leo, hatujaelewa vile mambo hayo yalinyamazishwa. Nina imani kwamba Serikali inawajua walanguzi wa dawa ya kulevya. Ikiwa haiwajui, hili litakuwa jambo la kushangaza sana. Watoto wetu Mombasa wanakufa; watoto wetu Mombasa wametufikisha mahali ambapo tuna hofu kwamba katika mwaka wa 2030, hatutakuwa na vijana wa kiume. Leo hii, wasichana wetu wanaachwa na waume wao kwa sababu ya mihadarati. Vijana wameoza na kudorora. Wao sio tegemeo. Kama dada yangu Elachi alivyosema, tunafaa kuanza mafunzo ya madawa haya katika chuo kikuu. Lakini mimi naona tukianzia mafunzo hayo katika vyuo vikuu, tutakuwa tumechelewa. Curriculum inafaa kuanzia shule ya msingi. Utumizi wa dawa hizi unaanza katika shule za msingi. Kuna watoto ambao tumewashuhudia wakila peremende za rangi ya blue . Ukiona ulimi wa mtoto ukiwa blue, unafaa kujua ni dawa hizo amekula. Serikali inafaa kutia maanani mambo haya. Wanaouza juices katika shule na vitu vingine vya kula, wengi ni walanguzi wa madawa ya kulevya. Kitu kinachotutia hofu ni kwamba wengi wanaohusika tunawajua lakini tukiwataja tunaweza kuwa kwa shida. Tarehe 30.12.2011, nilivunjiwa nyumba yangu kwa sababu nilikuwa katika kikundi ambacho kilikuwa kikipinga utumizi wa dawa za kulevya. Nilivunjiwa nyumba na kuharibiwa kila kitu. Ikiwa mihadarati inaingia nchini kupitia bandari ya Mombasa na kuna usalama, inaingia vipi? Ikiwa inaletwa kwa ndege na kuna usalama, inaingia vipi? Nina imani kwamba walanguzi wa madawa ya kulevya ni watu ambao wanafanya kazi katika Serikali katika ngazi za juu. Hili ni swala gumu. Tulipotazama kipindi cha Jicho Pevu, tuliona kwamba kimeangazia kila kitu kinavyofanyika. Leo, Serikali ikataka kujua Emma yuko aje, hawatakosa kunichunguza na kunijua. Wengine wanawekewa CCTV katika nyumba zao bila kujua. Mimi naamini kwamba Serikali inawajua walanguzi wa madawa ya kulevya lakini haitaki kuchukua hatua. Sisi kama kina mama, tunafaa kuchukua hatua na kuwa na njia mwafaka za kupambana na madawa ya kulevya. Nashangaa Chinedu atarudishwa bila kuhukumiwa hapa Kenya. Kwa nini kama sisi tunapopatikaka na makosa huko nje, tunahukumiwa huko na huko na kufungwa, kwa nini tunawasafirisha nje? Naunga mkono."
}