GET /api/v0.1/hansard/entries/385294/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 385294,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/385294/?format=api",
"text_counter": 43,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Hoja hii ambayo imependekezwa siku ya leo na Sen. (Dr.) Zani ni ya manufaa makuu kwa nchi yetu. Tuna bahati kwamba katika utawala wa mkoloni mzungu hakuweza kuyaondoa madini yote kutoka Kenya. Tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa jambo hili. Nchi nyingi za Bara la Afrika ziliporwa na wakoloni. Nchi yetu bado iko na rasilimali ya kila aina ardhini. Pia tuna rasilimali ya udongo mwema ambao hutumika na kampuni kubwa ambazo zinajihusisha na ukuzaji wa mimea kama vile tumbaku, miwa, mpunga na kadhalika. Hivi karibuni tumeona kwamba kuna wawekezaji wengine ambao ni wadanganyifu sana; mabepari ambao hawana shukrani. Wanachukua kila kitu ambacho wamekipata na kupeleka kwao. Mifano mingi ipo. Kwa mfano, ukuzaji wa tumbaku katika Mkoa Nyanza na hasa Kaunti ya Migori. Tumepata kampuni ambazo zinageuza majina kila baada ya miaka mitatu. Kampuni imeitwa British American Tobacco (BAT), baadaye Alliance One, na kadhalika kusudi wasilipe ushuru kwa Serikali. Tuna wawekezaji wengine kama Master Mind Tobacco (MMT) ambo huja na kudanganya watu na kuchukua mali na kuenda kuuza mahali peningine bila kurudisha mkono kwa wale ambo wamekuza zao hili wala hata kusaidia kujenga shule au zahanati. Bw. Naibu Spika, sheria kama hii ikiundwa, kwamba lazima asilimia kiasi fulani itengewe serikali za mashinani, ni vizuri sana. Sen. (Dr.) Zani amependekeza asilimia 20, itakuwa jambo bora, la heri na hekima kwamba tupate hizi pesa zikirudishwa mashinani kukuza uchumi wa sehemu hizo ili kuwe na shule, zahanati na viwanja vya michezo vizuri na pia kuwe na miradi mingi ya kuwasaidia akina mama. Bw. Naibu Spika, katika Kaunti ya Migori tumebahatika kuwa na dhahabu nyingi. Sen. Kajwang amesema tumepata wezi waliojificha kwenye mipango ambayo haiyeleweki. Wawekezaji wengine wanapata leseni kwamba wanakuja kuchunguza kilicho ndani na kuanza kuchukua mali hiyo miaka nenda, miaka rudi, bila kulipa ushuru kwa Serikali. Wanafanya hivyo kwa sababu ya rushwa. Hawa ni watu katika Serikali ambao wanahongwa ili wasiangaze macho na kuona uovu unaoendelezwa na watu hawa. Hawa ni wanafiki wanaohujumu uchumi wetu. Hili liwe jambo la kusahaulika kabisa kwa sababu miaka mingi imepita ambapo wananchi wameibiwa na wawekezaji. Wawekezaji hawa wamekuja nchini wakijifanya wamekuja kuchunguza na wanachukua mali na kupotea nayo. Hatutakubali jambo kama hili tena. Serikali za mashinani zinafaa ziwe angalifu sana. Ni lazima tuangaze sheria zote ambazo zimeandaliwa ili tuhakikishe kwamba rasilimali yote ambayo imeondolewa mahali fulani, jamii husika zimepata kiwango kidogo cha uchumi kusudi wakuze maslahi yao. Bw. Naibu Spika, hii ni sheria ambayo sidhani kama kuna Seneta ambaye ataipinga ingiwa tunajua ya kwamba si sehemu zote za Kenya ambazo zimebahatika kuwa na vitega uchumi kama hivi vya madini na kadhalika. Lakini kuna sehemu zingine ambazo zimebahatika kuwa na mbuga za wanyama au kuwa na sera nzuri za utamaduni wao wa kuanzisha nyimbo na michezo mizuri ambayo pia ni rasilimali ambazo zinatumika katika hoteli na kadhalika. Mambo ya angazwe na njia wakfu itafutwe ya kuona ya kwamba tunaweza kutega uchumi huu kwa namna gani. Tunapofanya hivi, tujihadhari kwa sababu tunaweze kuwafukuza wawekezaji ikiwa kodi itawekwa kiwango cha juu. Serikali tayari ina kodi ya mapato ambayo inafukuza wawekezaji. Sisi tusidai The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}