GET /api/v0.1/hansard/entries/385308/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 385308,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/385308/?format=api",
"text_counter": 57,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 758,
"legal_name": "Boy Juma Boy",
"slug": "boy-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kwanza ningependa kutoa shukrani kwa Sen.(Dr) Zani kwa kuleta Hoja hii. Maoni yangu ni kwamba Sen. (Dr) Zani alikuwa anafikiria juu ya Kaunti ya Kwale katika mawazo yake. Hii Hoja ni juu ya Kaunti ya Kwale. Lakini kwa sababu yeye ni Seneta mteule mawazo yake ni ya kitaifa. Mimi nitazungumza juu ya Kaunti ya Kwale. Hii ni moja kati ya kaunti maskini sana. Hata hivyo, ni moja kati ya kaunti zenye utajiri mwingi wa rasilmali. Tuna fuo zakuvutia sana. Mwezi wa Desemba, watu wengi kutoka bara huja kuogelea katika bahari yetu. Lakini watu wetu hawafaidiki hata kidogo na bahari na fuo zake. Bw. Naibu Spika, Kaunti ya Kwale inasambaza zaidi ya asilimia 30 ya maji yanayotumiwa katika Kaunti ya Mombasa. Maji haya hutoka Tiwi na Marere springs. Watu wa Mombasa ndio wanaopata maji mazuri lakini sisi watu wa Kwale tunatakikana tuwe wachafu. Hatufaidiki na maji haya. Bw. Naibu Spika, tuna mbuga za wanyama. Mfano mzuri, ni Shimba Hills National Park ambayo ni kilomita 30 kutoka Leisure Lodge. Katika mbuga hii kuna wanyama wengi kama vile ndovu, nyati na simba. Lakini watu wa Kwale hawapati chochote kutokana na shughuli za kitalii katika mbuga hiyo. Hata kaunti haipati ndururu. Sisi watu wa Kwale tumebarikiwa na madini. Na hii siyo siri. Hatukuomba kuwa Wakwale ni Mwenyezi Mungu aliyetuweka katika kaunti hii. Tuna madini kama vile titanium, dhahabu, rubi na kadhalika. Kwanza tuzungumzie hili swala la madini maanake The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}