GET /api/v0.1/hansard/entries/385310/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 385310,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/385310/?format=api",
    "text_counter": 59,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Seneta amesema kwamba asilimia 20 ipewe kaunti. Ninamuunga mkono kwa sababu asilimia 20 inapewa kaunti ya Kwale kunakotoka madini. Je, pale mjini kwenye kile kijiji kunakotoka madini, watu wa kutoka pale ndio watakaohamiswa makwao; wale ndio watapatikana na zile shida za mazingira, lakini hawapati chochote. Kwetu sisi kuna kampuni inayoitwa Base Titanium ya kutoka Australia. Watu wamehamishwa baada ya Base Titanium kuwalipa watu vizuri. Wakati huu, madini ya titanium yanaendelea kuchimbwa. Base Titanium imejenga shule na hospitali. Tunalia kwamba wale wenyeji wa pale si wanaopata kazi kwa sababu hawana digrii. Watu wetu hawakusoma. Wataalamu wote wanaofanya kazi hapo ni Wazungu. Mkaazi au mwenyeji wa Kwale hapati chochote. Anaona watu wakizunguka na magari makubwa ilhali hana chake. Hali yake ni ile ile, siku nenda, siku rudi. Sasa faida ya kuwa na yale madini ni nini? Ninawaonea huruma wenzangu Waturkana; kama hali hiyo itakuwa hivyo kule kwao, basi itakuwa mafuta ni jina tu. Hawatapata faida yoyote. Ni lazima wale watu wanaotoka eneo lile lenye madini wafaidike. Wapate nafasi za kazi. Kampuni hii ya Titanium iko pale Mrima. Watu wanaofanya kazi huko wanatoka mahali pengine. Kenya ni yetu sisi sote. Hata hivyo, ni lazima tuwafikirie wenye madini. Sikatai nchi ya Kenya ni yetu sote. Lakini mnatufukuza katika mahali penye madini bila kutufikiria sisi. Jambo hili huleta balaa. Kuna madini ambayo yako hapo yanayoitwa Rare Earth na Niobium . Madini haya ni ghali sana. Kila mtu sasa anataka kwenda Mrima. Lakini watu wa Mrima wenyewe hawapati faida yoyote. Ninaunga mkono kaunti yenye madini itengewe asilimia 20 na watu wa Mrima wapate haki yao. Ikiwa Serikali itachukua asilimia moja, je, watu wangapi wa Mrima watafaidika? Hakuna hata mmoja. Tunasema kwamba wale watu wa Mrima wafaidike kwa nza, kisha Kaunti ya Kwale na nchi ya Kenya kwa jumla. Hata sisi ni Wakenya kama Wakenya wengine wote. Kama ni hospitali au shule wajengewe kwanza. Ni lazima watoto wao wapewe busary ili wajiunge na vyuo vikuu. Haifai sisi kuzungumza juu ya madini, ikiwa ugavi wake hautawasaidi wenyeji. Ni aibu kuna watu wanaolinda madini wakiishi katika hali ya umaskini. Hawana chochote. Ni maskini hohehahe. Hali hii haikubaliki, ndio maana mnasikia wengine wakisema kwamba “Pwani si Kenya”, kwa sababu wameonewa. Hii ni Kenya ya aina gani? Kwa mfano katika Mombasa Port, asilimia 70 ya wafanyakazi hawatoki Mkoa wa Pwani. Si huu ni ukabila? Huu ndio ukweli wa mambo. Kwani ni pwani pekee ndipo kuna mashirika ya umma tu? Ukweli usemwe hata kama unauma. Hata kama unakasirisha, ni lazima usikie ukweli. Mashirika haya ya umma yako Nairobi, Kisumu, Nakuru, Kakamega na kwingineko. Mashirika hayo yanawafaidi watu wa sehemu hizo. Haya ndio mambo yanayoleta utata. Utata huu ndio unafanya hii young generation ya akina Hassan kutokubali mambo haya kwa sababu hao ni digital . Ni kwa sababu ya hali hii ndio ninaunga mkono Hoja hii. Ninasema Hoja hii ina umuhimu na itekelezwe vile ilivyo. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono kikamilifu Hoja hii."
}