GET /api/v0.1/hansard/entries/385667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 385667,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/385667/?format=api",
"text_counter": 69,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1029,
"legal_name": "Ali Abdi Bule",
"slug": "ali-abdi-bule"
},
"content": "Nashukuru Bw. Spika. Mimi nikiwa nimechaguliwa kutoka Tana River, jambo la barabara likigusiwa, kwanza, ninashtuka kwa sababu kwangu ni kama kulisahaulika kwa muda mrefu. Hivi nikisimama, watu wa Tana River wameaangalia kwangu; kuna sehemu ambapo kutoka enzi ya Kenya kuanza miaka 50 iliyopita, utaona kilomita 160 ambazo kwamba kuna wananchi karibu 10,000 walionipigia kura, na hakuna barabara, hakuna hospitali, hakuna usaidizi wowote ambao wanaweza kupata. Watu hawa ni wafanyi biashara; watu hawa ni wakulima; watu hawa ni Wakenya kama wengine, na hakuna barabara hata ile ya murram. Kwa hivyo, naunga Hoja hii mkono ili Kenya iwe sawa na barabara ziweko katika kila sehemu ya Kenya kama wengine. Asante, Bw. Spika. Naunga mkono Hoja hii."
}