GET /api/v0.1/hansard/entries/385706/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 385706,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/385706/?format=api",
"text_counter": 108,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, asante kwa kunipa nafasi kuunga mkono Hoja hii. Janga la maji na mafuriko limetuletea maafa mengi nchini. Mkoa wa Nyanza kwa sababu ya mto Nyando na kuja hadi Migori, tumepoteza watu 74. Mkoa wa Bonde la Ufa umepoteza watu 40 kwa sababu ya maji. Sehemu ya mashariki ya Kenya watu 21 wamepoteza maisha yao. Kaunti ya Tana River imewapoteza watu saba, Nyanza yenyewe kuna watu 19 ambao waliathiriwa na wako hospitalini. Hawa ni wale ambao wamehesabika. Watu wengi wamekufa maji bila idadi yao kujulikana. Shule nyingi zimeharibika. Zahanati nyingi zimeoshwa na mimea mingi mashambani kuharibiwa. Kila mwaka, tunakumbana na janga hili. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}