GET /api/v0.1/hansard/entries/385708/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 385708,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/385708/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Sen. Musila amesema si kwamba hatujui baada ya El Nino huja La Nina . Misimu hii hubadilika baadaya ya miezi kadhaa. Tunajua kwamba baada ya miezi mitatu au minne ni lazima kuwe na mafuriko. Lakini sisi kazi yetu ni kulia tu. Nafikiri wakati mwingine Mungu anashangaa na tabia za Wakenya. Hii ni kwa sababu wakati wa kiangazi tunamulilia Mungu na kusema: “Mungu tafadhali tuondolee janga hili la jua, kuna maafa” halafu analeta mvua. Lakini mvua inaponyesha tunalia na kusema: “Mungu tuondolee mvua hii sababu inatuua”. Nafikiri Mungu anashangaa na tabia zetu. Sisi hatuangalii mazingira yetu na kuyahifadhi. Ni lazima tuhifadhi maji ya mvua ili tuyatumie wakati wa kiangazi. Hata hivyo, tufuate mfano wa wananchi wa nchi kama vile Misri. Wao hutumia janga la garika kupata mawazo bora katika mashamba yao. Wakati kuna garika watu huwa wanahamishwa kwa sababu wanajua kwamba mahali hapa ni pa garika. Kwa hivyo, msimu wa masika umefika, tafadhali hameni na mwende nyanda za juu . Lakini sisi limekuwa kama jambo la biashara. Wakati fulani watu wa Budalang’i walianza kulalamika kwa sababu dyke zimejengwa kwamba hawatapata misaada kutoka kwa Serikali na mashirika mengine. Yaani hakutakuwa na garika. Kwa hivyo, imekuwa ni biashara na msimu wa kuvuna kutokana na mavuriko. Wanangojea wasombwe na mavuriko ili wapata misaada ya chakula na mablanketi kutoka kwa Shirika la Msalaba Mwekundi. Tabia mbovu kabisa! Kila wakati mtu anajua kwamba hapa ni mahali ambapo hujaa maji lakini kazi yake ni kujenga hapo kusudi maji yanapokuja, Mbunge aitwe, wakati huu nadhani Seneta aitwe kama kwamba nyinyi ni ATM au mitambo ya pesa kila wakati. Ukikosa kutoa pesa, kura zinaenda. Bw. Naibu Spika, tunacheka hapa lakini wajue kwamba wanapojaribu mambo kama hayo, wanaweka maisha yao hatarini. Wakati mwingine wakitarajia Mbunge afike, kifo kitabisha hodi. Pengine watakuwa wamempoteza mtoto, mzee, mama ama hata kuku. Na baadaye wanalia kama yule mama. Ajabu ni kwamba huyo mama amewekwa kwa televisheni kila msimu wa masika. Msimu ujao atatafutwa na wanahabari. Alianza tabia hii ya kulilia Serikali akiwa msichana mdogo, sasa yeye amezeeka na anaendelea na tabia hi. Huo ni upuzi na uzembe wa sisi Wakenya. Lakini tunapoangaza macho yetu kwa garika bila kufanya lolote, udongo wenye rutuba unazidi kusombwa na maji. Hiyo pia ni garika ya aina yake. Huo ni mmomonyoko wa udongo. Ni lazima pia tuhakikishe watu wanaoishi sehemu za milimani kuna usalama wa kutosha. Si vizuri kwao kulima karibu na milima kwa sababu ya kukatika kwa ardhi ambako kunaweza kusababisha maafa. Kwa hayo machache, ninaunga Hoja hii."
}