GET /api/v0.1/hansard/entries/385718/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 385718,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/385718/?format=api",
"text_counter": 120,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": ". Shida yetu ni kuwa nyumba zetu na mijengo mingine hujengwa bila mipango yoyote. Nilipokua nikiingia hapa, nilimsikia ndugu yangu, Seneta Musila akisema kwamba yeye alikua mkuu wa wilaya mwaka wa 1975 huko Tana River. Majanga haya yalikuwa yakitokea kila mara. Ukiyaona ya Musa, bila shaka utayaona ya Firauni. Mimi nilikua mkuu wa wilaya Kisumu. Maji ya Mto Nyando yalikuwa yakiwasomba watu, watoto, nyumba na mimea katika sehemu za Ahero na Nyabondo. Mimi mwenyewe nakumbuka nilichukua dau dogo ili kujaribu kwenda kuwasaidia watu, lakini kumbe nilikua naenda kuzama."
}