GET /api/v0.1/hansard/entries/385720/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 385720,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/385720/?format=api",
"text_counter": 122,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tuligonga miti ambayo hatukujua ilikua pale hata tukakwama hapo kwa muda wa masaa manne, hadi tulipokuja kuokolewa. Kweli, jambo hili si geni; ni jambo linalofanyika kila wakati. Kwa hivyo, ni lazima tuwe na mipango na mbinu za kuweza kukabiliana na majanga kama haya. Bw. Naibu Spika, wakati nilipokua katika Wizara ya Ulinzi mwisho wa mwaka jana, nilibuni shirika la Kenya Engineers Corporation. Shirirka hili litafanya kazi na mashirika mengine yasiyokukwa ya kiserikali. Natumaini ya kwamba wanajeshi wahandisi watapewa pesa za kutosha ili waweze kurekebisha mituta ama dykes kila pahali ili kuhakikisha kwamba maji yanazuiliwa yasiwasombe watu kwa kujenga mabwawa makubwa. Bw. Naibu Spika, ingawa hili janga la mvua linaletwa na Mwenyezi Mungu, hata sisi wenyewe tuko na makosa tunayofanya. Shirika la Uzalishaji Umeme la KENGEN linaachilia maji katika Bwawa la Kindaruma bila ya kuwapa watu wanaoishi nyanda za chini notisi. Wakulima wengi katika Kaunti ya Garissa wamepoteza mifugo na mali mengi. Wale wakulima wachache waliokubaliwa kulima kando kando ya mto kwa kutumia pampu za maji wamepanda mimea kama miembe, machungwa na ndimu. Jambo la kuhuzunisha ni kuwa kila mwaka pampu zao zote za maji husombwa na mafuriko. Jambo hilo hilo linafanyika katika Tana River. Wakati umefika Serikali kuilazimisha KENGEN kulipa ridhaa kwa wananchi ambao wanapoteza mali zao bila ya wao kupenda. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono."
}