GET /api/v0.1/hansard/entries/386116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 386116,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386116/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 758,
"legal_name": "Boy Juma Boy",
"slug": "boy-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ningependa kuungana na wenzangu na Seneta aliyeleta Hoja hii ya Usalama. Usalama ni mojawapo wa haki ambazo Mkenya anatakikana apate anapokuwa katika nchi yake. Sasa imekuwa ni jambo la kawaida kutokuwa na usalama. Utasikia swala hili likizungumziwa kule Mombasa, Kwale, Bungoma na kwingineko nchini. Hata hivyo, katika Serikali kuna vyombo vinavyohusika na kuleta usalama nchini. Tuna polisi wa kawaida na majasusi ambao kazi yao muhimu ni kuchunguza kwa udani. Haya mambo tunayoyazungumzia leo hupangwa katika fikira za wanadamu kabla ya kutekelezwa. Watu hupanga mambo kabla ya kuyatenda. Tuliona katika runinga watu wakigonga madirisha na kuwalazimisha watu kuvua suruali walizokuwa wamezivaa siku iliyotangulia. Kitendo hiki kinamaanisha kwamba majambazi walikuwa na intelligence yao. Tuliona mwizi akimwamurisha mwenye nyumba kutoa suruali aliyoivaa jana. Walijua hata rangi ya suruali zilizovaliwa na wenye nyumba. Ni wazi kwamba tendo hili lilipangwa kabla ya siku hiyo. Tunasema kwamba kabla neno halijatekelezwa, kuwe na njia ambayo itahakikisha kwamba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}