GET /api/v0.1/hansard/entries/386118/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 386118,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386118/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "halitatendeka. Kwa maoni yangu, haifai maafisa wa polisi kuwa katika kituo kimoja miaka nenda, miaka rudi. Afisa moja anafanya nini miaka kumi Kaunti ya Bungoma? Kwa nini tusiwabadilishe kila wakati? Afisa kama huyo anajua njia ya kujitetea na anapohamishwa anarudi hapo mahali. Ana mbinu zake za kuhakikisha hajahamishwa. Huu unakuwa ni mchezo wa paka na panya; hakuna linalofanyika. Kwa hivyo, mahali panapokuwa na shida, maafisa waondolewe mara moja. Kama vile mwenzangu alivyosema, kama ni mlegevu, basi afutwe kazi. Wakati mwingi, afisa kama huyo akifutwa kazi, atasema kwamba kabila lake linaonewa. Mambo hayo yanaturudisha nyuma. Tulibalisha Komishina wa Polisi na tukawa na Inspekta Jenerali. Je, mabadiliko haya yamefika mashinani? Hayajafika. Tumebadilisha majina ya askari wa utawala lakini, je mambo haya yametiririka na kufika kule chini? Hakuna. Hali ni ile ile. Sisi kama Seneti jukumu letu muhimu ni kulinda kaunti zetu. Ikiwa kaunti zetu hazina usalama, basi nchi haina usalama. Hakuna haja yetu kuvaa tai nzuri na suti za halili ikiwa hakuna usalama katika kaunti zetu. Kwa kaunti kuwa sawa lazima usalama uwepo. Hilo ni neno la wazi na halina haja ya kujadiliwa. Kwa hivyo, kama Seneti, ni lazima tuchukue jukumu la kuhakikisha kwamba usalama wa raia wetu unalindwa vilivyo. Mimi nazungumza kutokana na tajiriba ya miaka mingi. Sehemu kadha wa kadha zimevamiwa katika Kaunti ya Kwale. Wakati huu tuna simu za rununu. Jambo la kuhuzunisha ni kuwa ukimpigia polisi simu kumwaarifu umevamiwa, anachukua masaa mawili kabla hajafika. Ikiwa polisi watachukua muda huo wote, je, kutakuwa na usalama kweli? Mwisho, ninaunga Mkono Hoja hii kwa kuwauliza wanaohusika na usalama, wafanye bidii zaidi. Usalama wanchi hii upewe kipaombele na Serikali hii."
}