GET /api/v0.1/hansard/entries/386240/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 386240,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386240/?format=api",
    "text_counter": 69,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Haji",
    "speaker_title": "The Senator for Garissa County",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika, kwanza, ningetaka kukupongeza wewe na Bw. Spika kwa kuchaguliwa kusimamia hii Seneti. Sina shaka, kwa muda ule tumeweza kukaa pamoja, kuwa ninyi wawili ni watu ambao wanaweza kutuongoza katika kazi muhimu ya Seneti hii. Pia, ningependa kumpongeza Kiongozi wa chama tawala pamoja na kiongozi wa upinzani, wasaidizi wao pamoja na Chief Whips kwa kuchaguliwa kwao. Tunataka kuwahakikishia kuwa tutafanya kazi nao ili tuboreshe kazi ya Senati hii. Bw. Naibu Spika, pia, ningetaka kumpongeza Mheshimiwa Rais na Naibu wake kwa kuchaguliwa kwa wingi na wananchi wa nchi hii. Ningetaka kuwaambia kwamba kila mwananchi katika Kenya ana matumaini makubwa kwa juhudi watakazofanya kuweza kuboresha maisha ya kila mwananchi katika sehemu zote za Kenya. Ningependa pia kuwapongeza Maseneta wenzangu kwa kuchagulia na kuteuliwa. Sisi kama wazee ambao tumekuwa Bungeni mbeleni, tunawakaribarisha na tunafurahi kuwa pamoja nanyi. Bw. Naibu Spika, ningependa kuwashukuru watu wangu wa County ya Garissa kwa kunichagua kwa kura nyingi ambazo hazijawahi kuonekana katika Kaskazini Mashariki na Upper Eastern."
}