GET /api/v0.1/hansard/entries/386246/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 386246,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386246/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, Hotuba ambayo ilitolewa na Mheshimiwa Rais ilikuwa ya kufana sana. Iligusia matatizo mengi ambayo yanatukabili sisi kama wananchi wa Kenya. Ningetaka kuanzia umuhimu wa amani. Hakuna nchi ama binadamu yeyote ambaye anaweza kuendelea kwa njia yeyote bila kuwa na utulivu unaotokana na amani. Inaonekana ya kwamba amani katika nchi yetu inazidi kuzorota kila wakati. Katika sehemu nyingi za nchi hii, wananchi hawana raha kwa sababu ya ukosefu wa amani. Bw. Naibu Spika, hasa ningependa kuzungumza juu ya mambo ambayo yanafanyika katika mji wa Garissa. Wakati nilikuwa Kaimu Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani, haya matatizo ya watu kuuwawa yalikuwa yameanza. Nilipokwenda huko nilikutana na watu na tulizungumza na maofisa wa Serikali. Tulipendekeza mabadiliko mengi sana. Nilipeleka askaris 100 katika mji wa Garissa na maofisa 200 wa General Service Unit (GSU) kule Dadaab ambako wakimbizi wako tukitarajia kwamba matatizo haya yatakwisha. Lakini inaonekana kwamba siku baada ya siku hali inazidi kuwa mbaya. Kwanza, ningetaka kumshukuru Rais kwa kuwatuma maofisa wakuu wa usalama katika nchi yetu kule Garissa ili kuona ni hatua gani zinaweza kuchukuliwa ili haya matatizo yaondolewe. Lakini kwa bahati mbaya, askari wengi wamepelekwa hapo mjini. Ukweli ni kwamba yule mtu ambaye anakaa katika mji na ni mhalifu anayetafutwa, si kuku ambaye amefungwa miguu na kukaa pale.Atatafuta njia yoyote ya kuweza kutoroka. Anaweza kutoroka kwa miguu au njia yoyote ile. Kwa hivyo, suluhisho sio kuwapeleka askari wengi kwenda kuwasumbua raia na kuwapiga. Hasa sisi tuna culture na dini. Hata ukisoma the Public Health Act, utaona ya kwamba wakati unataka kwenda kufanya inspection ya nyumba ya Mwislamu, kwanza, unawaambia wanawake wa- withdraw ili utekeleze operesheni hiyo. Kwa hivyo, badala ya kufanya operesheni hiyo kwa utaratibu na njia nzuri ya kupata usaidizi wa wananchi, inaonekana ya kwamba wananchi watakasirika zaidi na kuogopa hata kutoa habari kwa Serikali. Kwa hivyo, hilo sio suluhiso mwafaka. Serikali ingebuni tume inayoongozwa na majaji kwenda kule Garissa kufanya inquiry na kujua chanzo cha jambo hilo ni nini. Kama ni mambo ya Al Shabaab, kama vile ambavyo tunaambiwa, Mandera ni less than 200 metres kutoka kwa mji unaoitwa Bula Hawa ambao unashikiliwa na Al Shabaab, na matatizo haya hayapo kule Mandera. Nimezungumza na Gavana wetu wa Garissa leo na amenieleza ya kwamba operesheni ambayo inafanyika katika mji wa Garissa haiwezi kutusaidia, bali itawafanya watu wasiwe tayari kuisaidia Serikali. Watu wa Garissa ni lazima wanajiuliza wenyewe: Je, inawezekana mtu kuvua suruali na kuhara katika"
}