GET /api/v0.1/hansard/entries/386250/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 386250,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386250/?format=api",
    "text_counter": 79,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "na kwingineko, maji yanawabeba watu. Maji haya yanaweza kuhifadhiwa kwa kutengeneza dams kubwa kubwa ili kuweza kufanya irrigation. Isitoshe, sisi wakaazi wa County ya Garissa tuko juu ya Tana River. Watu wetu, kwa sababu ya ng’ombe na ngamia kuisha na ukame kila wakati, wangetaka kufanya ukulima. Lakini wakaazi wa Tana River ambao wanadai kwamba huo mto ni wao, hawatukubalii sisi tutumie maji hayo kufanya irrigation. Hilo ni jambo ambalo Serikali inatakikana kuchunguza. Ningeomba kwa haraka iwezekanavyo Serikali iuunde Tume ya mipaka ili kusuluhisha matatizo ya mipaka katika Garissa na Coast Province. Hii ni kwa sababu kama kungekuwa na mipango ya irrigation kando ya mto huo wa Tana, maji hayo hayangeweza kuwafikia watu hao na kuwauwa. Isitoshe, maji hayo yanaenda kwa bahari, na huku unazuia mwananchi wa Kenya kuyatumia kulima na kukuza mimea na kusaidia nchi nzima ya Kenya. Kwa hivyo, Serikali ikitaka kufanikisha mambo ya irrigation, inafaa kuangalia utaratibu wa kujenga mabwawa makubwa katika sehemu kame ambako kuna ardhi yenye rotuba. Isitoshe, matunda kama mapapai, ndimu, ndizi, maembe na mananasi yanayokuzwa kule ni matamu sana kuliko yale ambayo yanatoka katika sehemu baridi. Bw. Naibu Spika, kuhusu tourism, kama vile mwenzangu alivyozungumza, kuna wanyama wengi katika sehemu kame katika nchi yetu. Ni jambo la kusikitisha kusikia kwamba watu wanawauwa vifaru na ndovu ilhali tunajua ya kwamba uchumi wa nchi hii yetu unategemea sana mambo ya utalii. Hata Rais katika hotuba yake amesema kwamba watafanya bidii kuona kuwa idadi ya watalii wale ambao wanakuja kutembelea Kenya itaongezeka. Kuna mwenzangu mmoja aliyezungumza hapa – nafikiri alikuwa ni Sen. Billow Kerrow – na kusema kwamba watalii hawa hawaji kuona vile sisi ni wafupi, warefu, wanono au vile wasichana wetu ni warembo. Wanakuja kuwaona ndovu na vifaru. Kwa hivyo, kuwaachia watu binafsi kuwahifadhi wanyama hao ni hatia kwetu kama nchi. Bw. Naibu Spika, nimeambiwa ya kwamba watu ambao wanawauwa wanyama hawa siku hizi wanatumia bunduki inayoitwa silencer. Ikirusha risasi hata mtu aliyekaribu hawezi kusikia. Nilisema kuwa sio kawaida kwa raia binafsi kuwa na bunduki za silencer. Niliambiwa kuwa watu hawa wana teknolojia ya kuweza kutengeneza silencer yao wenyewe. Kwa hivyo, biashara ya kuwauwa ndovu na vifaru itazidi kuendelea na huenda ikazorotesha uchumi wetu kwa sababu watalii hawataweza kuja. Kwa hivyo, ningeomba Serikali iweke hata homeguard mmoja kwa vifaru wawili ama ndovu kumi, kuwachunga usiku na mchana ili tuwanase wawindaji haramu ambao wanawauwa hawa wanyama. Bw. Naibu Spika, nikiangazia mambo ya kaunti, ningependa kuwaambia viongozi wa county assemblies, magavana na hata sisi wenyewe, Maseneta, kuwa kwa muda mrefu tumelia juu ya ukosefu wa maendeleo kwa sababu tuliamini kwamba wale ambao walikuwa wanatoa uamuzi kutoa pesa za maendeleo hawakuwa watu wetu. Leo tumepewa kisu na mbuzi ili tuweza kumchinja sisi wenyewe, kutoa ngozi na kugawa nyama hiyo. Kwa hivyo, lile jambo kuhusu “marginalization” ambalo watu wengi wamezungumzia, halifanyiki katika county yetu."
}