GET /api/v0.1/hansard/entries/386253/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 386253,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386253/?format=api",
"text_counter": 82,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kuwapongeza Maseneta wenzangu kwa uteuzi wao. Sen. Haji alichaguliwa na watu 50,000 ilhali nilichaguliwa na watu 200,000 katika Migori County. Ninawashukuru watu wa Migori kwa sababu waliweka ukabila kando, ikiwa ni sehemu kubwa ya kabila la Wajaluo na kunichagua mimi kuwa Seneta wao. Ninawashukuru na ninaahidi kuwatumikia vilivyo. Bw. Naibu Spika, sio wakati wote kukebehi wala kutojali Hotuba ya Rais. Ninafikiri ilikuwa nzuri na ilisomwa kwa ufasaha, uadilifu na kwa lugha ya Kiingereza sanifu bila kusita na kwa muda mzuri. Letu sisi ni kusema kwamba aliyoyasema yatekelezwe; isije ikawa ni hekaya za Abunuasi wala hadithi za Alfu Lela Ulela. Inafaa atie aliyoyasema maanani kwa sababu sisi tukiwa kwa upinzani tutafuatilia kwa dhati hatua hadi hatua kuona kwamba kweli Hotuba yake ya kwanza imetekelezwa vilivyo. Na akifanya hivyo, huenda akatushawishi wengine kuwa wafuasi wake. Lakini asipofanya hivyo, atawapoteza wengine njiani. Rais alisema kwamba atasikiliza siasa za upinzani na kwamba hana shida na jambo hilo. Alisema kwamba yeye ataangalia Serikali za ugatuzi na kuheshimu yaliyowekwa katika Katiba kwa sehemu hiyo. Lakini nilitarajia kwamba baada ya kusema hivyo angesema kwamba makomishna wote wahamishwe mara moja kwa sababu Katiba haiwapi huwo uwezo wanaojitakia. Alishindwa kusema jambo hilo labda kwa kupenda au kwa kusahau. Alisema kwamba ataangazia sehemu zote za Kenya kwa kutekeleza mambo ya hali na mali iliyo sawa. Lakini ukiangalia yaliyoandikwa leo katika gazeti la Nation wameorodhesha majina 150 ya Wakenya ambao wanataka kuteuliwa kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara. Inafaa uangalie majina hayo yametoka katika sehemu gani ya Kenya hii. Migor iliyo na watu milioni moja imepata nafasi moja tu, ilhali Mkuria hayumo, Ogiek hayupo na sitaki kutaja wengine. Sasa ukorofi waanzia hapo kwa sababu hizo sehemu sasa zimebaki kwa utuezi wa Makatibu hao na sio vizuri. Lakini kikapu cha mzee huwa kina mengi. Labda tukisahauliwa hivyo, atateua wengine. Bw. Naibu Spika, Rais alisema kwamba ataunda Baraza la Mawaziri wachache na ndio akaanza jana. Aliwatangaza Mawaziri wanne. Katiba inasema kwamba kila Waziri lazima awe na ujuzi, kisomo cha kutosha na uzoefu kwa Wizara hiyo ambayo atatekeleza kazi yake. Ukiona Wizara ya Afya, Rais ameteua mtu asiye na ujuzi kabisa, kwa sababu kazi yake ni kwenye benki. Mimi nikiwa mmoja wa madaktari Kenya hii, tunaona hii ni dharau. Angechukua mmoja wetu kuwa Waziri wa Afya. Tuna wasomi wengi ambao ni madaktari na wana ujuzi wa utawala wa hali kama ilivyo. Siwezi kusema sababu zake lakini hiyo ni dosari ambayo ni lazima aone kabla hajatangaza Mawaziri waliobaki katika Wizara zile zingine 14. Kila Mkenya yu macho na atasoma kile ambacho Rais wa nchi hii, kijana mwenye nguvu, atafanya. Tunatarajia mengi. Ni mengi yamesemwa hapa; mambo ya utawala, usalama na mimi pia niliguzwa na mambo ambayo Seneta mwenzetu alisema jana kwamba alikuwa mzima lakini sasa ni kilema. Sen. Haji amesema mengi yanayotendeka kaskazini mwa nchi ya Kenya. Na sio hivyo tu, hata kusini kule Migori County ambayo inapakana na Trans Mara na hata ndani ya County ya Migori yenyewe, kuna jamii ambazo zinapigana sio kwa sababu wanapenda kupigana, lakini kwa sababu wale maofisa wa Serikali ambao wako pale wamekaa hapo miaka mingi kuzidi kifani; zaidi ya miaka kumi. Kwa wakati huu kazi yake imekuwa ni kupokea rushwa tu. Hana kazi nyingine. Anafurahia maiti za wananchi akila rushwa. Ni kwa nini wasihamishwe? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}