GET /api/v0.1/hansard/entries/386255/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 386255,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386255/?format=api",
"text_counter": 84,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, mambo yanayoendelea kaskazini mwa Kenya ni kwa sababu ya rushwa. Hivi juzi wamejaribu kuwahamisha maofisa wale ambao wamekaa hapo siku nyingi, lakini hilo sio suluhisho. Ukachero unatakikana ufanywe mashinani kwenye wazee wa nyumba kumi kumi ili watoe taarifa kwa Serikali kuu kwamba leo tuna mgeni ambaye ameingia hapa asiyestahili na ambaye sisi hatumfahamu. Sera kama hii imeleta ufanisi na amani kwa nchi jirani. Ukienda Ethiopia au Tanzania, wazee wao wa nyumba kumi kumi sio wazee tu bali wengine wamefundishwa mambo ya Serikali na ulinzi. Mwaka jana tulipitisha katika Bunge kwamba wazee hawa walipwe; wapewe mshahara. Hatujui kama hilo jambo litatekelezwa au limepitwa na wakati. Usalama ni muhimu kwa sababu bila usalama basi yote ambayo ameyasema hayawezi kutekelezwa kabisa. Alipogusia elimu alisema kwamba kwa siku 100 zijazo, tutaona mengi. Alisema kwamba watoto wachekechea watapewa tarakilishi. Hivyo ni vizuri, lakini hao watoto wanajua nini? Je, watapewa ile tarakilishi tunatumia hapa ama watapewa kinyago (toy) tu? Kwa sababu wao wanajifunza kwa kuangalia picha, afadhali, angesema atatoa toys kwa watoto wa darasa la kwanza kwa sababu hiyo ndiyo lugha inayoeleweka. Kwa hivyo, sisi tunangoja tuone kweli kabisa kwamba hizo laptops ambazo zitatolewa zitakuwa za aina gani na zitagharimu kiasi gani cha fedha. Sisi Wabunge tumeshtakiwa kuwa walafi na kujitakia makubwa kwa kuitisha mishahara mikuba ilhali pesa zinapotea kupitia njia kama hiyo. Bw. Naibu Spika, wenzangu wamependekeza kwamba kuwe na nyumba moja ya tarakilishi chache, na ninafikiri ninaunga mkono yale yalioyosemwa na Sen. Khaniri. Sisi tunaona kwamba hili jambo linaweza kufurahia au la kumcheka Rais baada ya siku 100. Sisi tutacheka! Lakini hata hivyo, mambo ya elimu ni kwamba sehemu zote za Kenya haziko sawa. Kuna sehemu zingine ambazo zina walimu waliopita kifani. Kwetu nyumbani unapata madarasa manane ya wanafunzi 900 yakiwa na walimu watatu. Ikaja sera ya Serikali ya kutufunika uso kwamba wameanzisha shule za kitaifa vijijini kusudi sisi tusione zile shule nzuri nzuri ambazo zimejengwa mahali kwengine zikiachiwa wenyewe. Huo ni ubepari mamboleo kwa sababu elimu haipeanwi kwa usawa katika sehemu zote za Kenya. Kwa hivyo, sehemu zingine zitabaki nyuma siku zote. Ugatuzi umefika na tumeambiwa kwamba tutapewa pesa kulingana na vile tulivyo; County 47, lakini tusisahau ya kwamba kuna sehemu zingine katika nchi ya Kenya ambazo zimejiandaa na zina viwanda, barabara nzuri, hospitali nzuri na kadhalika. Viwanda vinatoa ushuru na kuna wafanyikazi ambao wanatozwa ushuru. Serikali hizo zitakuwa na pesa zaidi kuliko serikali za ugatuzi zingine na watapiga hatua kubwa mbele. Tujihadhari kabla hatari hii itokee. Bw. Naibu Spika, juzi, tulionyeshwa kwamba sehemu zingine hazina hata benki. Watu wanauza mifugo lakini hawana benki ambapo wataweka rasilmali zao. Je, viwanda vitatekelezwa namna gani? Rais ameongea sana juu ya viwanda ilhali kule kwetu tunalima tumbaku. Tukishalima hiyo tumbaku inawekwa kwa malori na kupelekwa kule Thika ambako kuna kiwanda. Ni nani anayefaidika? Yule anayelima hawezi hata kuajiriwa kwenye kiwanda hicho. Huu ni ukoloni Mamboleo. Tuna madini kila mahali lakini wale wenye rasilmali katika sehemu zao, je wamefunikiwa vizuri kuona kwamba faida wameipata? Pia kuna wafugaji wa mifugo ama wakuzaji wa vyakula. Ukienda Marakwet, utapata maembe mengi sana yakimwagika chini na kuoza ilhali watu kutoka eneo hilo wanakufa kwa ufukara kwa sababu hawana The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}