GET /api/v0.1/hansard/entries/386363/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 386363,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386363/?format=api",
    "text_counter": 63,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chiaba",
    "speaker_title": "The Senator for Lamu County",
    "speaker": {
        "id": 3,
        "legal_name": "Abu Mohamed Chiaba",
        "slug": "abu-chiaba"
    },
    "content": " Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuungana pamoja na wenzangu na kutoa shukrani zangu, kwanza kabisa kwa wale watu ambao walinichagua katika Kaunti ya Lamu. Walifanya hivyo kwa kipindi kirefu na hivi sasa ni heshima kubwa kuwa mimi ndio Seneta wa kwanza baada ya Katiba mpya kuwa implemented. Bw. Spika, nataka vile vile kuchukua fursa hii kuwapongeza Maseneta na Wabunge wote waliochaguliwa, wakiongozwa na Rais wetu ambaye alichaguliwa kwa kura za kutosha. Hapa kwetu katika Seneti, nataka kukupongeza wewe, naibu wako na wale wote ambao wamepata fursa ya kuweza kutuongoza sisi. Bw. Spika, tukiangazia yale yanayofanyika katika kaunti zetu, ni wajibu wetu sisi wenyewe ambao tulichaguliwa kuweza kusema yale mengi yaliofanyika na yale mengi ambayo hayakuweza kufanyika kwa njia moja au nyingine. Ikiwa kiongozi anaweza kusema yale ambayo hayakufanyika, kama infrastructure, hasemi ya kwamba anapinga Serikali yake. Anasema vipi inaweza kurekebisha mambo ambayo hayakupatikana kwa miaka 50. Ikisemekana ni kweli ya kwamba katika Kaunti ya Lamu nzima hakuna barabara ya lami hata inchi moja, hiyo ni kweli na itabakia kuwa ukweli, iwe imezungumzwa na upinzani au watu wanaounga mkono Serikali. Hivi sasa kila mahali watu wanategemea serikali ya ugatuzi au county governments ipatiwe madaraka ya kutosha iweze kuwa ndio suluhisho ya mambo mengi ambayo hayakupatikana. Katika Lamu kwa miaka miwili au mitatu iliyopita tunapongeza Serikali kwa kuleta mradi mkubwa wa LAPSET. Lakini hata hivyo, hiyo vile vile imekuja na matatizo yake mengine. Watu ambao hawajulikani katika Kaunti yetu ya Lamu ndio wamepatiwa mashamba makubwa makubwa ya kutosha, kinyume na kuchukua nafasi ya kuweza kuwapatia wenyeji walioko huko. Watu wanaoishi katika Lamu Kaunti ni wa Kenya nzima; ni wa makabila tofauti tofauti na tunakaa kwa amani. Ingefaa ikiwa wale ambao wamekaa kule kwa miaka mingi wangepewa haki. Mimi ninaunga mkono mradi huo mkubwa. Tunaona ya kwamba mradi huo ndio suluhisho tu ya kuweza kuleta kazi kwa vijana wetu na mabadiliko ya kiuchumi katika Kaunti hiyo na kaunti jirani. Bw. Spika, nampongeza Rais kwa yale mengi aliyoyasema katika Hotuba yake ambayo alitoa katika kikao cha pamoja cha Bunge letu. Tunampongeza kwa miradi ambayo yeye mwenyewe amependekeza na mikakati ya kuonyesha ya kwamba atapeleka maendeleo katika kila upande wa Kenya ambao haukufikiwa. Hilo ni jambo ambalo kila mtu anafikiria. Wajibu wetu mkubwa kama viongozi wa kitaifa ni kuiambia Serikali The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}