GET /api/v0.1/hansard/entries/386379/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 386379,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386379/?format=api",
    "text_counter": 79,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senator for Kilifi County",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuwashukuru watu wa Kilifi Kaunti kwa kunichagua kama Seneta wao wa kwanza. La pili, pia vile vile ningependa kukupongeza kwa kuchaguliwa kama Spika wa Seneti. Pia, ningependa kuwapongeza Maseneta wenzangu kwa kuchaguliwa kuwa Maseneta. Katika Hotuba ya Rais, alizungumzia kuhusu kutofautiana kwa maoni na kuheshimiana. Ningependa kuongea juu ya mambo ya utalii. Ile Kaunti ambayo ninawakilisha hapa Seneti ina hoteli nyingi kuanzia Mtwapa mpaka Tana River. Hoteli hizo hutembelewa na watalii wanaotoka katika sehemu nyingi sana za nchi za ng’ambo. Watalii wanaokuja katika nchi yetu, baadhi ya wale wanaotembelea mbuga za wanyama na kutupa income tax, kunao wengine, katika sehemu ya Mtwapa na Malindi ambao sio watalii bali huja kufanya biashara. Biashara zao zingine ni zile za mihadarati na ngono. Hao ni watalii ambao hawaleti faidi kwa nchi hii. Katika ile Kaunti ninayowakilisha hapa ndani ya Seneti, kunao wafanyikazi ambao wanawachishwa kazi; kazi ambazo wanaandikwa bila kufuatilia sheria za wafanyikazi. Wakati mwingine, hali ya binadamu wanapoishi wawili wakiwa wameoana ama wakiwa hawajaoana, ni lazima mmoja apate mimba. Hali hiyo ikitokea, tunaona kwamba wafanyi kazi wengi katika hoteli nyingi huko Pwani, wanawachishwa kazi. Wanawake wanapotungwa mimba, wanawachishwa kazi. Rais, katika Hotuba yake alisema atazingatia mambo ya utalii vilivyo. Pia, tunaomba sheria za wafanyikazi ziangaliwe vilivyo. Kunao wengine pia ambao The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}