GET /api/v0.1/hansard/entries/386381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 386381,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386381/?format=api",
    "text_counter": 81,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wanawaandika watu kazi halafu malipo yanakuwa chini kuliko kiwango ambacho kinafaa kulipwa kulingana na Sheria zetu za Kenya. Jambo lingine ningependa kutaja ni lile la beach boys na beach girls . Hawa ni wafanyikazi ambao wanafanya kazi katika ufuo wa bahari. They are an industry tothemselves . Hawa huleta watalii wengi katika Kenya yetu. Lakini utaone wale wanaofanya kazi kama beach boys ama beach girls wanateswa, wanashikwa, kufurushwa ama wanapelekwa kortini bila kuzingatia sheria. Wakiwa na vibali vyao ambavyo wamekata, wamelipa pesa na wameruhusiwa kuifanya biashara hiyo, basi ingekuwa vyema kama wangepewa nafasi ya kufanya kazi bila kusumbuliwa aidha na Kenya Wildlife Services (KWS) ama Kenya Tourists Police (KTP). Kama ni kuuza vinyago, nguo ama sanamu za mbali mbali, wanafaa kufanya hivyo bila kusumbuliwa. Jambo lingine ambalo ningependa kugusia ni lile la mashamba. Katika Hotuba ya Rais katika ukurasa wa 15, aligusia allisema kwamba ataangalia mambo ya mashamba na Serikali itaangalia vile itasuluhisha swala la mashamba. Kama inavyojulikana, Kaunti ya Kilifi inaongoza kwa kuwa na maskwota wengi katika nchi nzima. Jambo hili halikuletwa na kitu chochote kingine isipokuwa mabepari walionyakuwa ardhi ya wakaazi wa Kilifi County. Ardhi hizi zilinyakuliwa kwa kutengeneza makaratasi katika Lands Registry; makaratasi ya uongo ambayo hayana hati kikamilifu kisheria. Swala hili liliwafanya watu wa Pwani na hasa watu wa Kilifi kuwa na mchafuko na damu kumwagika hasa wakati wa uchaguzi. Hili ni swala la kusikitisha kwa sababu heshima sio utumwa. Watu wa pwani kwa sababu ya ukarimu wao umekuwa ni wakati wa kulipisha ardhi zilizonyakuliwa. Ikiwa Serikali iko na mwelekeo wa kisawasawa, basi tuna matumaini kwamba mashamba yalionyakuliwa yataregeshewa wenyewe ambao walivurushwa kutoka mashamba hayo. Jambo lingine la kusikitisha ni kwamba wakaazi wa Kilifi County hasa wale wa Mji wa Mtwapa -- Mtwapa ni jiji ambalo linajengwa usiku na mchana. Watu wanazidi kuwa wengi. Hii ina maanisha kwamba biashara pia inazidi kuwa nyingi. Leo, ni aibu kuona kwamba lile shamba ambalo lilikuwa limetengwa ambalo liko kati kati ya Mtwapa limechukuliwa. Limenyakuliwa na vipari ambao wananyakuwa mashamba. Hilo shamba ni la Serikali na ni la kujenga soko. Hili ni shamba ambalo ni la wafanyakazi wadogo wadogo ambao wanauza kando ya barabara ili waweze kupata nafasi hiyo ya kuweza kuuza bidhaa zao. Ardhi hiyo ilikuwa imetengwa kwa ajili ya kujenga soko lakini kumekuwa na watu ambao wamenyakua na wana nia ya kuanza mjengo. Ikiwa Serikali hii iko na nia ya kuona kama kuna mipangilio kabambe ambayo itaweka wakaazi wa Kilifi haswa wale wafanyi biashara wadogo wadogo wa Mtwapa katika hali nzuri ya biashara basi ichukue hatua ya kuhakikisha ya kwamba wale mabepari wa kunyakua mashamba wawache kufanya yale wanayofanya ili wafanya kazi wadogo wa biashara wapate ardhi hiyo. Serikali ya ugatuzi ambayo iko chini ya Kaunti ya Kilifi ikiongozwa na Gavana iweze kujenga soko ili watu wapate nafasi ya kufanya biashara hapo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}