GET /api/v0.1/hansard/entries/386383/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 386383,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386383/?format=api",
"text_counter": 83,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika vile vile tuko na mambo ya Giriama Ranch. Ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba hili ni shamba la ekari zaidi ya elfu tatu. Lakini kuna watu wametengeneza makaratasi ya uongo na wakapeleka kwa benki na hivi sasa shamba hilo ambalo liko na wakaazi wa huko upande wa Ganze wamefurushwa. Ikiwa Serikali iko na nia, kama vile anavyosema Mhe. Rais, basi shamba hili la Giriama Ranch liweze kurejeshewa Wagiriama wenyewe ili waweze kulisha mifugo wao na wapate maendeleo yao. Ningependa pia kuzungumzia swala la ukabila na nafasi za kazi. Tangu tupate Uhuru, Rais wa kwanza Hayati Kenyatta, Rais wa pili Mzee Moi na Rais wa hivi juzi aliyeondoka mamlakani, Mzee Kibaki, hawakuzingatia hali ya kupeana kazi kisawa sawa haswa kwa wakaazi wa Pwani. Wakaazi wa Pwani wamekuwa watu ambao si Wakenya. Wamekuwa watu ambao nyadhifa za kazi zikitokea katika Serikali za juu hawapewi nafasi hizo ama hawaangaliwi hata ikiwa wamesoma. Kwa hivyo, ikiwa Serikali hii inazingatia wakaazi wa Kilifi na Pwani kwa ujumla, tungependa kuona watoto waliosoma wakipewa nafasi katika nyadhifa za Serikali. Bw. Spika, jambo la mwisho ni hili. Nataka kumpongeza Rais na ndugu yangu, William Ruto, ambaye ni Makamu wa Rais. Si ndugu yangu wa kuzaliwa lakini ni kama rafiki na mtu ambaye ninamfahamu. Nataka kuwapongeza kwa msimamo ambao wamechukua kwa sababu wale watu ambao wamewachagua wanaonekana kama watu wenye taalumu waliosomea hizo wizara. Lakini pia vile vile hata tukisema “mgalla muue na haki yake mpe”, hawa wawili tutakuwa tunawapiga tochi kuona ya kwamba watu wa Pwani tunatarajia uongozi huu utakuwa tofauti na ule uongozi wa rais wa kwanza, wa Moi na wa Kibaki, kuona kwamba watafungua ukurasa mpya na watu wa Pwani watapata nafasi za kazi za juu katika Serikali. Ningependa pia kugusia upande wa barabara. Hali ya watu wa Kilifi na Pwani kwa ujumla kukinyesha mvua kunakuwa na mafuriko na magari hayawezi kwenda huko. Hata mahali ambapo pangekwenda kwa muda wa dakika tano kunachukua karibu masaa mawili ama matatu kufika. Ninapozungumza hivi, ninagusia hali ya kusikitisha kwamba watu wangu wa Ganze ambapo ni ndani kama kilomita 40 hivi na hakuna hospitali ambayo inazingatia hali ya akina mama wakiwa waja wazito. Kwa hivyo mtu akiwa katika hali hiyo, inabidi apelekwe mpaka Kilifi District Hospital. Huu ni mwendo ambao ungechukua dakika kumi na tano lakini kwa sababu barabara si nzuri---"
}