GET /api/v0.1/hansard/entries/386411/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 386411,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386411/?format=api",
    "text_counter": 111,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Nyakeriga",
    "speaker_title": "The Nominated Senator",
    "speaker": {
        "id": 13112,
        "legal_name": "Linet Kemunto Nyakeriga",
        "slug": "linet-kemunto-nyakeriga"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, nashukuru Katiba ya sasa ya Kenya kwa kuwakumbuka walemavu. Ni mara nyingi ambapo tumefikiria sisi tutakumbukwa lini lakini sasa tunashukuru sana kwa sababu tumekumbukwa. Nikirudi katika Hotuba ya Rais, hii ilinifurahisha sana. Tulipoona kwamba tulikumbukwa kama walemavu, hakika tulifurahi. Nikianzia na swala la elimu, jambo la elimu kwa mtoto mlemavu limekuwa ngumu sana. Lakini kwa wakati huu, tumefurahi kwa sababu tumeona kwamba tunakumbukwa. Tunahitaji vifaa kama vile brailers,scratches na vingine vingi. Tunaomba kwa sababu Serikali imetukumbuka, wakati inapopeana tarakilishi, nasi pia tukumbukwe wakati huo. Pili, katika mambo ya tarakilishi, naona ninaweza kuwasaliti lakini sio sana kwa sababu nilipozaliwa sikuwa nikiona lakini nilipomaliza kusoma shule ya nursery nilijua kusoma brail na kuandika. Kwa hivyo, hiyo ni changamoto kwamba tarakilishi zinaweza kufanya kazi. Wanafunzi wanaweza kutumia laptops katika masomo yao. Mimi ningependa kusema kwamba laptops zinaweza kutumika na watoto wetu."
}