GET /api/v0.1/hansard/entries/386415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 386415,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386415/?format=api",
    "text_counter": 115,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "nafasi ili tufanye kazi na Wakenya wenzetu na tutafurahia. Tunapokosa nafasi, tunajihisi kwamba tuko katika nchi tofauti. Lakini sasa, kwa kuwa mmetukumbuka, tunajua ya kwamba sauti yetu imesikika. Kwa kuongezea, nakumbuka kwamba kuna watu walemavu wengi ambao hawawezi kusonga kutoka mahali walipo. Kwa hivyo, pia hao wanahitaji kushughulikiwa. Katika upande huo wa facilities, ningependa tuwakumbuke ili tuwatoe mahali walipo, vitandani, ili nao pia wafurahie kama vile wengine wetu wamefurahi. Mimi kama Linet nimetembea na kufika hapa. Je, yule ambaye hawezi kusonga, tutamsaidia aje? Kwa hivyo, nina shukuru kuwa katika Jumba hili la Seneti. Ningeomba tusaidiane kama Maseneta ili nami pia niweze kuwa na muda mrefu wa kushugulikia wengine ambao hawawezi kufika hapa. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, ninashukuru na kuunga mkono Serikali hii ya sasa."
}