GET /api/v0.1/hansard/entries/386435/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 386435,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386435/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "The Senator for Taita-Taveta County",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kwanza, nakupongeza kwa kuchaguliwa kama Naibu Spika wa Seneti. Pili, nachukua fursa hii kuwashukuru sana wakaaji na wenyeji wa Kaunti ya Taita Taveta ambao wamenipa nafasi hii kuwa Seneta wao wa kwanza kuambatana na Katiba mpya. Pia ninawashukuru sana watu wa Voi ambao walinichagua kuwa mhe. Mbunge wao muhula uliopita. Ningependa kumshukuru Rais Kibaki aliyestaafu majuzi na Waziri Mkuu kwa kunipa nafasi kuwa Waziri katika Serikali yao. Bw. Naibu Spika, ninachukua nafasi hii kuwapongeza wenzangu waliochaguliwa na walioteuliwa na vyama mbalimbali kuwa Maseneta wa kwanza katika Seneti hii. Bw. Naibu Spika, ninataka nizungumzie kwa kifupi Hotuba ya Rais ya tarehe 16/04/2013. Hotuba yenyewe ilikuwa nzuri kwa sababu ilijaa ufasaha na malengo mengi. Mhe. Rais na naibu wake ni viongozi wa kizazi cha kisasa. Wao wanaamini kusema na kutenda. Wakati huu wamesema mengi na tunataka kuona matendo yao. Hii ni kwa sababu imani bila matendo haifai. Mhe. Rais alitaja nguzo muhimu sana katika Hotuba yake. Nitazungumzia kwa kirefu juu ya nguzo ya utaliii kwa sababu nilikuwa Waziri wa Utalii katika Serikali iliyopita. Mimi niliona furaha kubwa wakati mhe. Rais wa nchi ya Kenya aliposema idadi ya watalii wanaokuja hapa inaweza kuongezeka na kufikia milioni tatu. Utalii unaleta takriban Kshs100 bilioni kila mwaka. Lakini Wizara au shirika llinalopewa pesa za kuuza au kutangaza Kenya nje linapewa Kshs400 milioni. Kiasi hiki cha pesa ni cha chini sana. Ni lazima tumulishe nyasi ng’ombe anayetupa maziwa. Itakuwa bora zaidi kama Serikali hii itaangazia utalii kwa undani na kutenga takriban asilimia tano ya pesa inayokusanya kila mwaka. Ikiwa sekta hii inaleta Kshs100 bilioni kila mwaka, basi tuipe zaidi ya Kshs5 bilioni. Wakipewa pesa hizo, basi wanaweza kuuza Kenya duniani kote na watalii wengi watazuru hapa. Ni lazima kuwe na usalama nchini ili tuweze kuwavutia watalii wengi. Kila wakati nilipokuwa nikisafiri nje ya Kenya, jambo la kwanza lilikuwa ni kutangaza Kenya. Ninajua hata wewe Naibu Spika ulipokuwa balozi, watu wengi huko nje walipenda kujua hali ya usalama hapa nchini. Tumekuwa na ukosefu wa usalama hapa nchini kwa muda mrefu. Tunakubuka kila baada ya wiki moja au mbili, ikiwa si mlipuko wa bomu, ni wa guruneti. Watu walikuwa wakipigana kila mara. Kwa hivyo, ikiwa watalii watakuja kwa wingi ni lazima kuwe na usalama wa kutosha. Hakuna mtu anaweza kutembelea nchi jirani kwa starehe ikiwa katika nchi hiyo kuna vita. Usalama ni kigezo muhimu katika utalii. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}