GET /api/v0.1/hansard/entries/386437/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 386437,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386437/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Utalii wetu hutetegemea sana bidhaa mbili. Nazo ni wanyama pori na fuo za bahari kule Mombasa. Sisi tunatangaza mbuga za wanyama sita peke yake, ilhali tuna zaidi ya mbuga 60. Wakati umefika kwa yule atakayechaguliwa kusimamia sekta hii ahakikishe kwamba zile mbuga za wanyama 60 ambazo hazitembelewi na watalii zinatangazwa vilivyo. Bw. Naibu Spika, kumekuwa na changamoto nyingi baharini. Nilisikia mwenzangu akisema hapa kwamba wavulana na wasichana pale ufuoni wapewe nafasi ya kufanya biashara zao. Lakini mtalii anayekuja Kenya anataka kuona bahari na kuogelea ndani yake. Hataki kuiona bahari kwa mbali kwa sababu ya vijana hawa. Changamoto imekuwa ni kwamba wengi wanaofanya biashara pale pia hufanya uhalifu. Ndio maana tunataka tukubaliane nao ili watengewe sehemu yao ya kufanyia biashara zao. Tunataka kumuona mtalii aliyekuja baharini akiweka kitanda chake baharini na kujivinjari. Usalama ni kipengee kikubwa ambacho kinaweza kuvutia watalii wengi hapa nchini. Mhe. Rais alisema ataimarisha usalama. Hata hivyo, nilikuwa ninatarajia kwamba katika siku 100 ataupa kipaumbele usalama wa nchi hii. Tuna askari wa kutosha lakini hawana magari wala vifaa vya kisasa. Ukienda kupiga ripoti kwamba umevamiwa wanakuomba gari au petroli. Hiyo haiwezekani. Inafaa tuwape vifaa vya kisasa na tuangalie jinsi wanavyoishi. Jambo la tatu na muhimu zaidi, tuwalipe mishahara itakayowasadia kuishi vizuri. Askari hawa hujitolea mhanga kulinda sisi na mali yetu lakini mishahara wanayolipwa ni chini sana. Akiumizwa akiwa kazini inafaa ashughulikiwe ipasavyo. Nimeona askari wengi wakienda hospitalini hawashughulikiwi vilivyo. Usalama ni kipengee kikubwa cha kuleta maendeleo. Tunaona vile hali kule Garissa na kwingineko inavyoendelea. Hali hiyo si ya kupendeza hata kidogo. Wakaazi wa eneo hili hawawezi kufanya biashara zao. Bw. Naibu Spika, ningependa kuzungumzia juu ya ugatuzi. Si mara ya kwanza tunao ugatuzi hapa nchini. Tulikuwa na ugatuzi katika Katiba ya kwanza 1963 hadi 1966. Na kilichofanyika wakati huo ndio kinachofanyika sasa. Serikali za ugatuzi za 1963 na 1966 zilinyimwa pesa. Ziliponyimwa pesa zilisambaratika. Serikali zile za ugatuzi zimeanza ilhali kufikia leo hazijapewa pesa za kutekeleza majukumu zake. Itakuwa vigumu kama tutaendelea kusema tunataka ugatuzi ilhali tumewanyima pesa. Inafaa tuulinde ugatuzi kama Maseneta. Tulikuwa na Katiba kama hii ya leo mwaka 963 hadi 1966 lakini ilibadilishwa. Hofu yangu kama mpinzani ni kwamba Serikali ina waheshimiwa Wabunge wengi ambao wanaweza kubatilisha mambo mengi. Inajaribu wakati huu kuwashawishi waheshimiwa Wabunge wa Upinzani ili wajiunge nao. Isije ikawa ni njama ya kuua ugatuzi kama ilivyofanyika mwaka wa 1966. Kama vile wanavyosema wahenga: Ukiumwa na nyoka mara ya kwanza, ukiona mti barabarani, utafikiria ni nyoka. Sisi kama Maseneta ni lazima tutetee ugatuzi hapa nchini. Lakini ili tuwe na nafasi hiyo, ni lazima pia Maseneta waangazie zile ngazi katika Serikali na wawekwe mahali pao. Hauwezi ukawekwa nambari 43 na useme unaenda kutetea Gavana ama wale wengine ambao wako katika ngazi za juu. Tulizungumzia hayo na ni matarajio yangu kwamba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}