GET /api/v0.1/hansard/entries/386439/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 386439,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386439/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "tutarekebisha mambo hayo ili Maseneta wawe na nguvu zaidi kuambatana na Katiba yetu. Tunataka kumuona Seneta akiwa juu ya Gavana. Kuhusu malipo ya wazee, ninengependa kusema yalikuwako miaka mitano iliyopita. Katika miaka hiyo mitano, kulikuwa na ubaguzi. Kila eneo Bunge lilikuwa limepewa kata moja. Wazee kutoka kata hiyo walipata pesa hizo kwa muda wa miaka mitano iliyopita na wengine wakanyimwa. Hivyo basi, wazee wakaona kwamba Mbunge aliyekuweko - kama vile nilivyokuwa Mbunge wa Voi - alipendelea kata fulani. Kwa wakati huu, malipo haya yafanywe kwa utarartibu ili wazee wa miaka 55 na zaidi wapate pesa hizi kwa haraka ili watakoenda kaburini waende na sura ya furaha. Maanake ni lazima kila mtu ataenda kaburini. Lakini inafaa wapewe pesa hizi wakiwa hai ili ziwasaidie. Mhe. Rais alizungumzia juu ya ardhi. Hata kama kuna National Land Commission, sisi wakaaji wa Pwani, hasa kutoka Kaunti ya Taita Taveta, tunahisi kwamba kuna njama ya kutotekeleza masuala ya ardhi sawa sawa. Tunaomba Serikali hii chipukizi na inayoongozwa na vijana kwa haraka iweke mikakati kabambe ili shirika hilo liweze kufanya kazi kikamilifu. Kwa mfano, katika kaunti ya Taita Taveta, asimilia 62 ya eneo lote ni mbuga ya wanyama. Asilimia 28 ni mashamba makubwa makubwa, asilimia nne ni milima ya Taita Hills, ilhali wakaazi wa Taita Taveta wana asilimia sita pekee yake ya kulima na kuishi. Ni huzuni kuwa wakaazi hawa hawana stakabadhi za kumiliki mashamba yao. Ni aibu kubwa kwamba miaka 50 baada ya Uhuru tunaona kwamba asilimia sita ya kaunti nzima haiwezi ikagawanywa na watu kupewa stakabadhi za mashamba. Mhe. Rais alizungumzia shirika linalosimamia mambo ya mashamba. Shirika hili linafaa kupewa mamlaka haraka ili tupate stakabadhi zetu na ili tuwe kama Wakenya wengine. Katika Mkoa wa Pwani, watu wakiambiwa ukweli hawataki kuusikia. Suala la ardhi ni nyeti sana. Ni suala ambalo tunatake litekelezwe kwa haraka ili lilete uwiano baina ya watu wa Pwani na watu wa maeneo mengine ya Kenya. Watu wetu wanataka kujihisi Wakenya. Kati ya miswada ambayo Mhe. Rais anataka kuleta Bungeni, hakuna hata moja inayohusu mbuga za wanyama. Mswada huu umekuwa tayari lakini haujawahi kuwasilishwa Bungeni. Kwa miaka kumi ya Serikali ya mpito, nilisubiri mswada huu kuwasilishwa Bungeni lakini haukuletwa. Mswada huu ungekuwa kati ya miswada wanayotaka kuleta hapa ili watu wanaoishi karibu na mbuga za wanyama wa pori, wanapoumizwa kwa bahati mbaya, wapewe fidia sawa sawa. Wakati huu tunalia sana tukiona simba wakiuwawa kule Kajiado. Tunahuzunika kuona ndovu wakiuwawa kule Taita-Taveta na sehemu zingine za nchi. Wenyeji wa sehemu hizo wanasherehekea kwa sababu ndovu ni adui kwao. Mswada huu unapendekeza kuwa mtu akiuwawa kwa bahati mbaya, afidiwe na Kshs200,000. Akiumizwa, anapewa Kshs50,000 na pia mazao yake yatafidiwa. Wakati huu ukiumizwa, hakuna malipo ya maana. Mswada huo ungepewa kipaumbele na mhe. Rais kwa sababu uko tayari na ulijadiliwa na Baraza la Mawaziri lililopita. Inafaa tuupitishe mswada huu ili watu wanaoishi karibu na mbuga za wanyama, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}