GET /api/v0.1/hansard/entries/386441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 386441,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386441/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "wajue ni kiasi gani cha pesa watakachopata wanapoumizwa au kuuwawa na wanyama. Ni fidia gani watayopewa mifugo yao ikishambuliwa na wanyama au ni malipo yapi watakayopata mazao yao yakiharibiwa. Jambo hili halikufanyika wakati uliyopita. Ni matumaini yetu kuwa Waziri atakayehusika na mambo hayo, akisha pewa wadhifa huo, ataupeleka mswada huo Bungeni ili wanaoishi karibu na wanyama watapata motisha ya kuwalinda. Bila sheria hiyo, itakuwa vigumu. Jambo lingine ambalo ningependa kulizungumzia ni Katiba yetu. Sisi sote hapa tumeapa kuitetea, kuitekeleza na kuilinda Katiba ya nchi hii. Tangu Uhuru hadi sasa, kumekuwa na sheria mbili katika nchi ya Kenya. Kuna Sheria ya mabwenyenye na ya walala hoi. Mlala hoi akiiba kuku kwa sababu ya njaa, anafungwa miaka saba. Bwenyenye akiiba Kshs10 bilioni, tunamsifu na kumheshimu kama kiongozi. Tunataka Katiba hii iwalinde watu wote. Ukiwa jizi, basi unafaa kwenda jela kwa makosa yako. Ukiwa mtu wa kawaida na upatikane na makosa, ufungwe jela kulingana na sheria za nchi hii. Hatutaki kuona sheria ambayo inapendelea mtu kwa sababu anamjua mtu fulani, anatoka wapi nayeye ni nani. Tunataka haki ifanyiwe watu wote. Tunataka Katiba ambayo haitajali sura, jina,ukoo au kabila la mtu. Mwananchi akikosa, aadhibiwe kulingana na sheria za nchi hii. Ikifanyika hivyo, hata yule mama aliyenyang’anywa shamba lake atakuwa na uhuru wa kwenda kortini na kujitete vilivyo kuambatana na Katiba ya nchi hii.. Nikimalizia, nataka kutoa tahadhari kwa Serikali hii ifanye haki kwa kila mwananchi. Wakenya wana matumaini makubwa katika Serikali hii. Matumaini yao yatekelezwe. Tumeona Serikali nyingi zikitoaa hadi lakini ahadi hizi zinaambulia patupu. Waheshimiwa Wabunge wengi hawajui kwamba kuna kiwanda cha mbolea cha KenRen. Ni aibu kuwa kila mwaka katika Bajeti yetu kuna pesa ambacho zinatengwa kulipa mkopo uliyotimika kujenga kiwanda hiki. Hata hivyo, kiwanda hiki hakipo. Hiyo ilikuwa ni sakata ya kuiba pesa za raia. Tunajua Serikali ya kwanza ilitumia pesa nyingi kununua mashamba makubwa yaliyomilikiwa na wazungu. Tungependa kuona mashamba hayo yamerudishiwa wenyeji kwa sababu yalimilikiwa na watu wachache waliokuwa Serikalini. Jambo hili limechangia sana kuibuka kwa vikundi kama vile"
}