GET /api/v0.1/hansard/entries/386443/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 386443,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386443/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "na vingine ili kutetea haki zao. Vijana hawa si wahalifu. Wanataka kujua ni akina nani walionyakua mashamba yao kule Nyeri na kwingineko. Serikali ya pili ilipokuja, tuliona msakato wa kufionza pesa za wananchi katika Goldrenberg. Tuliona msakato wa kufionza pesa katika All Africa Games. Hata katika Turkwell Gorge, pesa zilipelekwa lakini watu wakawekwa mfukoni. Ni mpaka lini Wakenya tutavumilia mambo haya? Serikali ya mpito, tuliona ikihusika na sakata ya Anglo Leasing. Serikali ilipoteza pesa nyingi kupitia sakata hiyo. Tuliona pia pesa za elimu ya watoto wetu kutoka kwa wafadhili zikiporwa. Ziliibwa na hakuna hatua zilizochukulia dhidi ya maofisa waliohusika na sakata hiyo. Kwa hivyo, tunaipa Serikali ya sasa tahadhari na onyo mapema wasije wakaingia katika shimo ambalo wengine waliingia na kuzama. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}