GET /api/v0.1/hansard/entries/386445/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 386445,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/386445/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mradi wa Lamu Port-South-Sudan-Ethiopia Transport Corridor (LAPSET) ni mzuri sana. Lakini tusipojahadhari unaweza kuwa shimo ambako Serikali inaweza kupoteza pesa nyingi kama wengine waliotangulia. Suala la kuwapa watoto wetu mitambo ya komputa au laptops ni nzuri sana. Hatupingi kwa sababu ni lazima tuwe na mwanzo mpya ili tusonge mbele kama mataifa mengine. Hata hivyo, mradi huu usiwe ni shimo la kufionzia pesa za Wakenya. Mwisho ni kumtakia Rais wa Kenya afya nzuri na nguvu nyingi za kutekeleza aliyotuhadi. Tumeelezwa tangu mwanzo kuwa Serikali hii ni ya kusema na kutenda. Kusema wamesema na tumesikia. Sasa tunasubiri matendo. Sisi kama Upinzani, tutawakosoa ikiwa hawatatekeleza ahadi zao. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}