GET /api/v0.1/hansard/entries/387303/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 387303,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/387303/?format=api",
    "text_counter": 316,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 128,
        "legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
        "slug": "richard-onyonka"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii ili nichangie jambo muhimu kama hili kuhusu ugatuzi na mahali ambapo tumefika. Jambo hili limewakera wananchi mno lakini sisi kama viongozi katika Bunge hili, tumekuwa tukilizungumizia na kuna mambo fulani ambayo ningependa kusema. Hapa Bungeni, vyama vyote kama vile Jubilee na CORD, tunakubaliana sisi sote ni lazima ugatuzi uendelee. Hatuna tashwishi kuhusu vile hela za Serikali yetu zitagawanywa mashinani. Tunajua kuwa kuna tashwishi kuhusu vile hela kutoka kwa Serikali kuu zitaenda mashinani ambako magavana na wanaojishughulisha katika serikali za kaunti watakuwa wakizitumia. Kuna uovu mwingi. Hata mkaguzi wa hesabu amesema kuwa hana uwezo wakati huu wa kuangalia vile hela ambazo zinaenda kwa magavana zitatumiwa. Kwa hivyo, ni lazima tuende pole pole. Kama vile Wabunge wenzangu wamesema, ni lazima tuende pole pole. Katiba inasema kuwa ugavi wa mali katika serikali ya ugatuzi ni lazima uchukue miaka mitatu. Hala hala ni ya nini? Tumewapatia magavana Kshs210 bilioni. Katika eneo langu la Kisii, tuna maeneo tisa. Eneo la Kisii limepewa Kshs6.1bilioni. Ukigawa hela hizi kwa maeneo tisa, kila eneo litapewa Kshs450 million. Hii Kshs450 million kwa miezi sita, itatumika aje? Hili ndilo jambo ambalo sisi kama viongozi katika Bunge hili tunalizungumzia. Ningependa kuwasihi ndugu zetu Senators wajue kwamba hatuwapigi vita. Wengine wetu tukitoka hapa, tungependa kuenda kule juu pengine tuwe Senators kwa miaka ijayo. Pia, tungependa kwenda kule chini tukakae na magavana. Wengine wetu tungependa kuwa magavana. Hatutaki kuharibu sheria za nchi hii ili ukipewa kazi kama hiyo miaka ijayo, ushindwe kuifanya. Nia na haja yetu ni safi. Tungependa ugatuzi ufanyike mahali ambapo magavana wana utu, heshima na wanachunga mali ya wananchi. Pia, wahakikishe kuwa ugavi huu unafuata sheria na unaleta mawasiliano, maelewano na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}