GET /api/v0.1/hansard/entries/388436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 388436,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/388436/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Asante Mhe. Spika. Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyeleta Ronald Ngala kutoka pwani, akaleta Jomo Kenyatta kutoka Gatundu na akaleta Jaramogi Odinga kutoka Nyanza ili watunasuwe kutoka kwa nyororo ya ukoloni. Namwomba Mungu huyo aweze kutuleta pamoja ili tujinasuwe kutokana na nyororo ya ukoloni mambo leo. Mhe. Spika, Katiba ya nchi, kifungu cha kwanza, kipengele cha pili kinanipa uwezo na mamlaka ya kuzungumza juu ya sheria yoyote katika nchi ya Kenya. Mimi ni mwakilishi wa wananchi. Kifungu cha nne cha Katiba ya Kenya kinasema kwamba Kenya ni taifa huru. Mtoto wa darasa la nane atajiuliza, ikiwa Kenya ni taifa huru, itakuwaje Rais wa taifa na makamu wake watapelekwa katika taifa lingine kushtakiwa? Je, watoto wetu watafahamu uhuru ni kitu gani? Nina sababu ya kuunga mkono Hoja hii. Sababu ya kwanza ni kwamba, ili ICC ije itekeleze wajibu wake lazima taifa liiruhusu. Katika kesi ya Kenya, ICC ilialikwa na Kofi Annan."
}