GET /api/v0.1/hansard/entries/388437/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 388437,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/388437/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Mhe. Spika, nimesoma katiba ya nchi, kipengele cha kwanza hadi 264. Sikuona kifungu hata kimoja kinasema Rais akifanya makosa, ashtakiwe nje. Nitatoa changamoto kwa mwanasheria yeyote aniambie kutoka kipengele cha kwanza hadi 264 ni wapi sheria ya Kenya imesema Rais ashtakiwe nje. Ninavyoonelea, hivi ni vita vya kiuchumi. Hii ni kwa sababu Serikali ya Jubilee ina ndoto ya kuboresha uchumi. Leo wataondoa Rais and naibu wake ili uchumi wa Kenya usambaratike. Ninaona hivi ni vita ya kijamii kwa sababu baada ya vita vya 2007, watu wa Mkoa wa Kati na Bonde la Ufa walishirikiana na kuunda serikali. Wazungu wanasema choices have consequencies. Tuliambiwa hivyo na wale watu wanataka kuharibu jamii yetu. Hivi ni vita vya kisiasa. Rais aliyechagulia kidemokrasia hafai kufanywa hivyo. Sasa kina Kofi Annan na wenzake, hii ni fursa yao kuleta rais wanaemtaka ili watawale nchi ya Kenya."
}