GET /api/v0.1/hansard/entries/388438/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 388438,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/388438/?format=api",
"text_counter": 177,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Mhe. Spika, tukiwa viongozi wa nchi hii, hatutakubali dhuluma inayoendelea. Katika kesi ya Lubanga, tuliambiwa kwamba Lubanga hana hatia aende nyumbani. Baadaye kidogo, tukaambiwa Lubanga ana hatia na angefaa afungwe. Je, hii ni kesi ya sheria ama ni ya siasa? Juzi tuliambiwa Mhe. Ruto ahudhurie kesi wiki mbili na atawale wiki mbili. Baada ya majadiliano kidogo, tukasikia Ruto hafai kwenda nyumbani. Sione sheria hapa. Kama ICC ingekuwa na sheria, mauaji yanayoendelea Syria leo hayangekuwepo. Watu wanauawa kwa maelefu. Fatou Bensouda angekuwa huko. Kama ICC inatekeleza sheria ulimwenguni, ile dhuluma iliyotokea Libya, Fatou Bensouda angekuwa huko. Leo Obama anatuambia Kenya---"
}