GET /api/v0.1/hansard/entries/388454/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 388454,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/388454/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Mhe. Spika, kabla sijavurugwa nilikuwa ninasema Obama ametoa amri kwamba lazima Kenya ishirikiane na ICC. Kabla hujaongoza Kenya, kwanza jisajili kama mwanachama wa ICC ndiyo tuheshimu ICC. Mwisho, Fatou Bensouda alipokuja Kenya alibahatika kwenda kwa kambi ya IDPs. Huko aliulizwa swali moja: Nyumba zetu zimechomwa na tumepoteza mali, je mashahidi wako ni nani na sisi tuko hapa? Hili ni thibitisho kwamba mashahidi wa ICC wamepikwa, wakaiva na wakapelekwa kule. Ili Kenya isidhulumiwe zaidi ya hapa, ningeomba tupitisha hii Hoja, tujiondoe kwa ICC. Ahsante mhe. Spika."
}