GET /api/v0.1/hansard/entries/388573/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 388573,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/388573/?format=api",
    "text_counter": 312,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Abdi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 398,
        "legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
        "slug": "yusuf-hassan-abdi"
    },
    "content": "Ahsante Mhe. Spika. Kwanza kabisa, nataka kusema naunga mkono Hoja hii. Napinga Kenya kuwa katika ICC kwa sababu za kiitikadi. Mashujaa wengi walimwaga damu yao ili Kenya ipate Uhuru wake. Uhuru tulionao haukupatikana kwa urahisi. Hatukupata Uhuru kama zawadi kutoka wa wakoloni. Tuliupigania. Kwanza kabisa, nasikitika kukubali ICC nilipokuwa katika Umoja wa Mataifa huko New York. Nasikitika sana kwa sababu naona sisi sio dola huru. Pili, ni kwa sababu ya wale wamepoteza damu yao bure. Kupeleka kesi hii na matatizo yetu kule ICC ni makosa makubwa ambayo tangu mwanzo, nilionelea haifai. Lazima tukatae. Kwa hivyo, nafurahi kwamba nimeweza kupata fursa hii kuzungumza hii leo na kuliangalia swala hili. Kwanza kabisa, ukiangalia muundo, sera na mkabala wa ICC, ni mahakama ambayo haitafuti haki. Ni mahakama ambayo imeanzishwa kuadhibu wale ambao wanapinga maslahi ya nchi za magharibi. Kwa mfano, mahakama hiyo ilianzishwa na mataifa matajiri tu. Na wote ambao mpaka sasa wamefikishwa mbele ya mahakama hiyo ni kutoka nchi za Kiafrika. Unadhani nchi za magharibi zingekubali ikiwa kuna mahakama ambayo inasikiliza kesi za watu weupe peke yao? Watu kutoka Ulaya na watu kutoka Marekani! Wangesema tu mara moja mahakama hiyo ni ya ubaguzi wa rangi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}