GET /api/v0.1/hansard/entries/388574/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 388574,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/388574/?format=api",
    "text_counter": 313,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Abdi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 398,
        "legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
        "slug": "yusuf-hassan-abdi"
    },
    "content": "Lakini sasa hivi ukiangalia, wote wanaopelekwa katika mahakama hiyo ni watu weusi. Huwezi ukajiuliza hiyo kweli mahakama ina haki na usawa? Halafu, hebu tutazame mwaka wa 2002 wakati mahakama hiyo ilivyoanza kazi yake. Mamilioni ya watu wameuawa. Kule Afghanistani, mamilioni ya watu wamekufa. Kule Iraq, mamilioni ya watu wamefariki. Ukiangalia Chechnya, wamepondwa pondwa. Kule Palestina, kuna matatizo makubwa ya haki za binadamu. Watu wanauawa kila siku. Lakini kwa nini sasa hivi hiyo mahakama haijajipa wajibu wa kutafuta waharifu na makatili ambao wamewaua maelfu na maelfu ya watu katika nchi ambazo nimezitaja? Hiyo inaonyesha kwamba mahakama hiyo inatafuta watu wanyonge; nchi ambazo hazina uwezo wa kujisimamia. Angalia kwa mfano Sudan. Kwa miaka mingi, nchi za magharibi zilikuwa zikiangalia ugandamizi uliokuwa ukiendelea kusini mwa Sudan. Lakini mara tu Sudan ilipoanza kuuza mafuta yake kwa nchi ya Uchina, ndiyo wakaanza kufahamu kwamba watu wa Sudan Kusini wana haki. Na Sudan ikaadhibiwa kwa sababu ilikuwa imefanya makosa ya kupeleka mali yake katika nchi nyingine. Kwa hivyo, ni njama za ukoloni mambo leo. Sisi hatutakubali na ni wakati muhimu sisi tujiangalie, si kwa sababu tu viongozi wetu wamepelekwa katika Mahakama ya ICC. Lakini ni kwa sababu sisi tunataka kuusatiti tena Uhuru na utawala wetu na tuwe na Dola linaloheshimika katika dunia hii, ambalo liko na haki sawa ya kuangalia maslahi yake na maslahi ya wananchi wake. Haki za kibinadamu mara nyingi haziangaliwi huku. Ni mahakama ya kisiasa. Ni mahakama ya kisiasa; ni mahakama ambayo inataka kuwaadhibu wale ambao hawapendelewi na kwa hakika sioni sababu yoyote sisi tuwepo katika hali kama hiyo. Nafikiri Hoja hii inatupa fursa ya kunyakua tena uhuru wetu na kujiendeleza kama nchi ambayo ina maslahi yake."
}