GET /api/v0.1/hansard/entries/389260/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 389260,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/389260/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi Spika wa Muda, tangu tuanze mipangilio hii, kaunti zetu zimekuwa zikiendeshwa kiholelaholela. Ninajua kwamba kuna matarijio mengi sana na watu wengi wanasema kwamba wanataka ufadhili. Hata hivyo, bila ya sera maalum, matarajio yetu kama Wakenya hayawezi kupatikana. Kuna msemo wa Kiingereza kwamba “kama hupangi, unapanga kutofaulu.” Sisi tunataka kufaulu na kuafikia maazimio yetu. Hii ni Hoja ya hekima sana kwa sababu inashinikiza baraza la magavana kuwahimiza wenzao kuwa na mipangilio ya kimaendeleo katika kaunti zao. Wengi wanafikiria kwamba kaunti zitafungua fursa ya kuweka hazina na kuleta maendeleo bila kuwa na mpangilio fulani. Muweka hazina hawezi kuwa na imani katika kaunti fulani mpaka ajue mpangilio na ratiba ya maendeleo yao ili waweze kutoa mchango fulani wa kimaendeleo. Juu ya yote haya, ni lazima tuwe na mipangilio ya kitawala ambayo italeta maendeleo. Inafaa kuwe na uwazi kwa masuala ya utawala na kihazina . Mara nyingi kumekuwa na fikra kwamba ni lazima tumjue gavana fulani ndio tupate kandarasi au fursa ya kuanzisha kiwanda ama mradi wowote katika kaunti yake. Ninahimiza kila kaunti, kama vile tunavyoishurutisha Serikali ya Kitaifa kufanya jambo fulani, kuhakikisha kwamba imeweka mipangilio maalum ambayo itaweka uwazi utekelezaji wa masuala ya kiuchumi na rasilmali za kitaifa. Bi Spika wa Muda, sisi sote tuna maazimio ya kuleta maendeleo katika sekta tofauti za kiuchumi. Kwa hivyo, ni lazima wakati wa kuyatekeleza maendeleo haya, tuwe na mpango ambao utawahusisha watu wetu wote. Haiwezekani kusema kwamba mtu mmoja ndiye amewashinda wenzake wote kwa hekima. Kama wewe umechaguliwa kama gavana ama seneta, haimaanishi kwamba wewe ni bora kuliko wenzako wote. Inamaanisha kwamba umepewa fursa na uwezo wa Kiserikali kuweza kuandaa mikakati ya kimaendeleo. Ni lazima kupitia Hoja hii tuwahimize wale ambao ni washirika katika masuala ya mipangilio hii, wawahusishe watu wengi katika kaunti zao ili waweze kupata mawazo na fikra tofauti kuhusianana na mipango yao ya kimaendeleo. Hakuna yeyote kati yetu aliye na hekima na fikra zaidi kuwashinda watu wote katika utekelezaji wa jambo fulani. Kwa hivyo, ili kutatua vizingiti katika ugatuzi, ni lazima tuhakikishe kwamba kuna ushirika. Inafaa tuwahusishe wakaazi wote katika kila kaunti ili waweze kushiriki katika mipangilio hii. Mwisho, kama hujui kule unakotoka, huwezi kujua unakoenda. Sisi tumeona kwamba kila mtu anapanga katika hewa. Kwa mfano, kutaka kiwanda cha kuleta nguvu za umeme katika kaunti za Nairobi na Mombasa kwa sababu kuna takataka nyingi. Haiwezekani kupata maendeleo ikiwa tutaona jambo na kulirukia kiholela bila mipangilio thabiti. Wenzetu katika nchi za magharibi waliweka misingi thabiti. Amerika ina The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}