GET /api/v0.1/hansard/entries/389262/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 389262,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/389262/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "umaarufu kwa sababu, kwa mfano, jengo la White House na Capitol Hill zilijengwa kwa mipangilio ya kudumu zaidi ya miaka 100. Hapa kwetu, tumeiba nyumba za wakuu wa Serikali, viwanja vya ndege, vioo na kadhalika. Hata ile mipango iliokuweko hapo awali yote imesambaratika kwa sababu ya wizi na ufisadi. Kwa hivyo, tutaanza upya na maendeleo yatafanywa kwa ratiba fulani ya kifuata mipangilio fulani. Waswahili husema kwamba, ukiona vyaelea, jua vimeundwa. Wale wenzetu wa mataifa ya kimagharibi hawakuamuka siku moja na kupata maendeleo. Walijitolea mhanga na wakajenga taasisi zao. Baadhi yenu mkizuru nchi hizo mnapigwa na butwaa kuona mijengo ya kifahari. Mara nyingi sisi hupiga mijengo hiyo picha ilhali hapa Kenya, hupigi picha mijengo yoyote kwa sababu hakuna jambo la kuridhisha. Wenzetu wameendelea kwa sababu babu wao walikuwa na mipango. Sisi siku moja tutaitwa waanzilishi wa Kenya mpya. Leo mimi ni kijana, lakini sitakuwa kijana maishani yangu yote. Na siku moja tutakufa na tutataka historia yetu iandikwe kama watu tuliochangia Kenya mpya. Ikiwa tunataka kuwa na historia nzuri juu ya maisha yetu, ni lazima tuwe na mipango maalum ya kutekeleza maendeleo yetu. Kila mara tunawanakili wenzetu kama vile George Washingtone na J.F. Kennedy, ilhali hatusemi ni nini wenzetu hapa nyumbani walifanya. Hayo ndio masuala ambayo ni lazima tuweke. Hawa magavana ni magavana wa kwanza katika majimbo yao ya ugatuzi. Ikiwa wanataka kukumbukwa, ni lazima waweke mipango kabambe. Bi Spika wa Muda, sera hii ni ya kuhimiza kila mtu aweze kukaa chini na kuandika mipangilio ya kimaendeleo. Jambo hili ni la lazima. Sisi tunawahimiza, na mimi nina imani kwamba wale watakaofuata mwongozo huu, watapata ufanisi na watakumbukwa katika historia ya Kenya. Kwa hayo machache, ninamshukuru sana Sen. (Dr.) Zani kwa kuleta Hoja hii. Ninaomba kuunga mkono."
}