GET /api/v0.1/hansard/entries/389494/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 389494,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/389494/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Waswahili wanasema “haba na haba hujaza kibaba”. Hii inamaanisha kwamba Wakenya wanapaswa kujinyima ndiyo waweze kuwa na akiba ambayo itawasaidia siku za usoni. Kama walivyosema Wabunge wenzangu, familia nyingi ziliadhirika kutokana na wizi wa fedha zilizowekwa katika benki fulani, ambazo hivi sasa hazipo. Moja ya benki hizo, ambayo ilimuadhiri mtu mmoja niliyekuwa na uhusiano wa karibu naye, inaitwa Agrarian. Kutokana na mambo kama hayo, watu wengi walipoteza imani kwa benki kwa sababu benki zilionekana kudhibitiwa na watu waliokuwa na ushawishi wa kisiasa na ambao wangeweza kuwatapeli watu wengine na kutokomea mbali. Kwa kweli, baadhi ya wale ambao waliregeshewa hela zao, walitumia ushawishi wa watu waliokuwa na uhusiano wa karibu na wenye benki hizo."
}