GET /api/v0.1/hansard/entries/389495/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 389495,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/389495/?format=api",
"text_counter": 168,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Ukitathmini kulingana na jinsi Serikali yetu ilivyokuwa ikikopa pesa, utaona kwamba kwa kiasi kikubwa, miaka kumi iliyopita, imekuwa ikikopa zaidi kutoka kwa soko la fedha la humu nchini. Kwa hivyo, ni muhimu kuhakikisha kwamba Wakenya wanaendelea kuweka hela zao kwenye benki na mashirika mengine ya kifedha ndiyo Serikali yetu iweze kupata fedha za kufanyia miradi ya maendeleo. Hivi sasa kuna tetesi kwamba zile hela ambazo zinafaa kwenda kwenye serikali za ugatuzi hazitoshi, na inabidi serikali hizo zikope ili ziweze kuwa na miundo msingi thabiti inayoweza kuwaletea Wakenya maendeleo. Kwa kweli, kuna nafasi nzuri iwapo Wakenya wataweza kuwekeza hela zao katika benki na mashirika mengine ya kifedha ili serikali za ugatuzi zipate nafasi ya kupata hela na kujiendeleza. Pia ni jambo la kufurahisha iwapo jambo hili litaweza kupata afueni kutoka kwa Wakenya. Uchina ni nchi ambayo inaweza kukopesha mataifa tofauti hele nyingi sana kwa sababu watu binafsi katika taifa hilo huwekeza pesa zao kwenye benki."
}