GET /api/v0.1/hansard/entries/389746/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 389746,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/389746/?format=api",
    "text_counter": 158,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kumpongeza Sen. (Prof.) Lonyangapuo kwa Hoja hii. Mtu anayeitwa KPR ni askari ambaye amepewa kifaa cha kujitetea, kulinda amani na kuweza kuona ya kwamba watu wanaishi kwa amani. Lakini tunajiuliza ni kwa sababu gani watu hawa wanaopewa vifaa kama hivi hawalipwi mishahara. Ni mpango gani Serikali iko nayo kuona ya kwamba watu hawa wamelipwa mishahara? Kutolipwa mishahara inamaanisha kwamba watu hawa wanafanya kazi bure ilhali hii si kazi ya kanisa, bali ni kazi ya kulinda amani. Amani haiwezi kupatikana kule pwani ikiwa mashamba ya watu wa pwani yamechukuliwa na watu wa bara. Huo ndio ukweli wa mambo na huo ndio ukweli unaojulikana na kila Mkenya; ya kwamba watu wa pwani kuanzia ufuo wa Bahari mpaka kwenye barabara, hakuna hata mtu mmoja wa pwani anayeweza kusema kwamba hili shamba ni langu. Mashamba yote yamechukuliwa. Hii ni kwa sababu hapo awali tulipopata Uhuru, ilikuwa sheria kwamba Rais ndiye anayeweza kupeana shamba kama zawadi kwa watu wakioana kwa harusi ama zawadi kwa rafiki. Hili ni jambo la kusikitisha sana. Bi Spika wa Muda, sisi tunasema kwamba ikiwa amani itapatikana kule pwani ni lazima mashamba yetu yarudi kwa watu wa pwani wenyewe. Pia kazi ambazo zingefanywa na watu wa pwani zimenyakuliwa. Tunasema hivyo kwa sababu ni mashirika mangapi ya Serikali ambayo yako pwani? Na watu wangapi hivi sasa ambao ni wakurugenzi wa mashirika hayo katika pwani? Hatuna hata mtu mmoja tunayeweza kusema kwamba ni mkurugenzi wa shirika la Serikali katika Kenya hii. Tunauliza, je wale watu wa pwani, wana haki ya kuwa na amani ikiwa kazi zikipatikana haziwezi kupewa watu wa pwani kwa sababu wakurugenzi wa masharika hayo sio watu wa pwani? Kwa hivyo, ili amani ipatikane, ni lazima watu wa pwani wapewe kipaumbele kwa upande wa kazi. Ikiwa KPR itaundwa, basi watu wale wanaotakikana kuandikwa kule pwani ni lazima wawe watu wa pwani. Hatutaki kuletewa watu wengine. Tunajua kuna mipangilio mbali mbali ya kwamba watu kutoka kwengineko watajitambulisha kama watu wa pwani ili wapewe kazi hizo. Katika vijiji vingine vya kule ndani kama vile Ganze na Chakama, utapata watu wa kule hawataandikwa kazi; wataletewa watu kutoka kwengine kama KPR. Tunasema kwamba kama ni Ijara, watu wa Ijara wapewe kazi hizo ya KPR. Kama ni Kilifi, watu wa Kilifi wapewe hizo kazi za KPR."
}