GET /api/v0.1/hansard/entries/389758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 389758,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/389758/?format=api",
    "text_counter": 170,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mbura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13153,
        "legal_name": "Emma Mbura Getrude",
        "slug": "emma-mbura-getrude"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Pia ningependa kumpongeza Sen. (Prof.) Lonyangapuo kwa kuleta Hoja nzuri kama hii, hasa kwa mama kama mimi anayetoka pwani. Sen. Lesuuda ametaja jambo fulani ambalo limenigusa moyo sana na ndio nikasimama; kwamba kwa miaka hamsini tumeongea kuhusu maswala ya usalama na mpaka wakati huu bado tunaongea kuhusu mambo hayo hayo. Hii ni wazi kwamba kuna watu ambao wanafaidika na mauaji ya wananchi. Nikigusia kwetu Mombasa, kitu ambacho kinanishangaza ni kwamba utapata vituo vya polisi vipo katika maeneo yasiostahili. Vituo vyote katika Kaunti ya Mombasa vimewekwa kwenye eneo la watu matajiri. Hawa ni watu ambao wako salama na nje ya milango yao bado wako na security, wako na mbwa lakini vituo vya polisi bado vinawekwa kwenye eneo hilo. Kuna wale ambao wako na interest na maafa haya yanayotokezea. Wakati huu ndio mwanzo wa Kenya kuwa na Seneti, ni wajibu wetu kama Maseneta Kenya hii tushughulike. Haya yote hayakufanywa na serikali zilizopita. Ni matumaini yangu na ninaamini ya kwamba haya yote yatatatuliwa na Serikali ya Jubilee."
}