GET /api/v0.1/hansard/entries/389760/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 389760,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/389760/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Zamani nakumbuka kwamba ilikuwa mwananchi akiona polisi usiku atamkimbilia na atasaidiwa mpaka nyumbani. Lakini sasa si hivyo. Mwananchi akiona polisi na nyoka, heri akimbilie nyoka amuache polisi. Usalama umekuwa tofauti. Mwananchi akiona polisi ni kama ameona jini, shetani ama mhalifu. Mambo yamebadilika. Katika sehemu ya Pwani, usalama unakosekana kwa sababu ya vijana kutumiwa na wanasiasa. Nimesikia wenzangu wakizungumzia kuhusu Mombasa Republican Council (MRC) na mashamba, lakini mimi narudisha kidole kwa wenzangu. Wakati mkisema kwamba mashamba ya Pwani yamechukuliwa na wabara lakini nauliza Kamau atajua aje Giriama kuna shamba linauzwa kama si wewe, mbunge, umemwambia kwamba kuna shamba linauzwa huko? Onyango atajuaje kuna shamba linauzwa Malindi kama si wewe, mbunge kutoka Pwani, kumwambia? Adui wa mpwani ambaye anafanya tusiwe na usalama ni mpwani mwenyewe na viongozi. Hawa ndio waliharibu usalama wa Pwani. Kwa hivyo, leo kazi yao ni kusimama na kupiga vita Serikali ya Jubilee ilhali adui wa mpwani ni mpwani mwenyewe ambaye yuko CORD. Mimi nataka kusema kitu kimoja. Ndugu yangu, Sen. (Dr.) Khalwale, amesimama na kusema kwamba maswala ya insecurity Pwani yanaletwa kwa sababu ya vijana kuona kwamba wanadhulumiwa. Mimi ningependa kusema kwamba MRC hawajasababisha kutokuwa na usalama Pwani. Ni uongo. MRC si wahalifu. MRC hawajapiga mtu kwa sababu wamepokonywa mashamba. MRC wanaongea na mdomo na hawapigi wala hawaui. Mambo ambayo Sen. (Dr.) Khalwale ameongea ni ya kupotosha Wakenya. MRC si wahalifu na wapwani si wahalifu. Sisi wapwani huwa tunaongea. Mpwani akizidiwa sana, silaha yetu ni mdomo. Mimi ningependa kusema kwamba tusipotoshane hapa kwa maswala ya ardhi huko Pwani. Hata sasa inasemekana kwamba waliopewa title deeds ni watu ambao sio wapwani lakini sijaona wakitajwa hao ambao si wapwani."
}