GET /api/v0.1/hansard/entries/389762/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 389762,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/389762/?format=api",
"text_counter": 174,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Hassan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 431,
"legal_name": "Hassan Omar Hassan Sarai",
"slug": "hassan-omar-hassan-sarai"
},
"content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda kwa fursa hii. Mwanzo kabisa, ningependa kumpongeza mwalimu wangu katika Chuo Kikuu cha Moi ambaye wakati huu ni Seneta mwenzetu, Prof. Lonyangapuo. Hili swala la usalama kwa ujumla ni swala nyeti. Sisi tungependa kushinikiza Hoja hii tukijua kwamba tukitekeleza usalama kama haki nyingine--- ni haki za kibinadamu kwa sababu bila usalama, mtu hawezi kufurahia haki nyingine kama haki ya maisha na haki ya milki ya ardhi na raslimali. Kwa hivyo, ni lazima tuhakikishe kwamba tumeweka msingi wa usalama. Jambo la pili ni kwamba katika kuhakikisha kwamba tumempa mtu jukumu, ni lazima jukumu lije na mapato fulani. Kwa mfano, kama unalipa Sen. (Prof.) Lonyangapuo, basi unaweza kumwambia ni yapi majukumu yake. Lakini kuwacha watu na hiari yao bila kuwapatia kandarasi ya majukumu ama msururu wa majukumu, ni lazima mtu apate mapato aina fulani. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kuimarisha hali ya usalama. Haiwezekani katika Kenya yetu kujenga nchi yetu kwa kila wakati kwa mambo ya kujitolea. Kwa mtu kujitolea, hauwezi kusistiza mtu huyo kuajibika. Kwa hivyo, ukiweka mapato ama terms of reference utaweza kuhakikisha kwamba mtu anawajibika. Ninaunga mkono Hoja hii na tunataka kuhakikisha kwamba katika Kenya yetu tunaweza kupata usalama. Hili ni swala ambalo sisi tulilishughulikia katika Tume ya Haki za Kibinadamu. Usalama ni kiungo muhimu katika taifa letu. Ukiangalia ile hisia ambayo mtu anakuwa nayo kwa Serikali ni wakati ambapo Serikali hiyo imemhakikishia usalama wake."
}