GET /api/v0.1/hansard/entries/389764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 389764,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/389764/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Jambo la pili ni kwamba hawa ni watu ambao tunawapatia nguvu kwa njia ya bunduki. Ukipatia mtu bunduki, pia ni lazima umshike kwa jukumu fulani kwa sababu bunduki na uwezo unaweza kutumika kwa njia mbaya. Mimi naunga mkono Hoja huu nikijua kwamba ni hatua kubwa na ile ambayo inaweza kuimarisha usalama katika taifa letu la Kenya. Ningependa kumaliza kwa kusema kwamba swala la usalama sio swala la chama. Swala hili ni swala ambalo Wakenya wote kwa ujumla lazima wahusike katika kuimarisha usalama. Sio Pwani peke yake ambapo hakuna usalama. Usalama ni swala la kila sehemu nchini. Katika maeneo ya North Eastern Province, wengi wao waliipigia kura Serikali ya Jubilee lakini hakuna usalama. Sisi kama wafuasi wa CORD tuko na imani ya kupata usalama North Eastern, Samburu, Turkana na kote nchini. Kwa hivyo, tusilete mitikisiko ya siasa katika swala la usalama kwa kusema kwamba usalama upo ama umekosekana Pwani kwa ajili ya CORD ama Jubilee. Idara ya polisi ni lazima ipatiwe majukumu na iambiwe kwamba lazima waimarishe usalama na kuwe na uhifadhi zaidi katika maswala ya usalama. Maeneo ya Kisii ama Bungoma, usalama haupatikani kwa ajili ya chama. Pia Isiolo kulikuwa na ukosefu wa usalama na ilhali hiyo ni ngome ya Jubilee. Kwa hivyo, sio vyema kuleta siasa ya pesa nane. Sisi hapa ni watu ambao tumepigiwa kura, watu wakijua kwamba sisi ndio tunaleta maazimio yao katika Seneti hii. La muhimu ni sisi kushirikiana kama washikadau katika taifa la Kenya ili kuhakikisha tumeimarisha usalama. Hoja hii imeletwa na Sen. (Prof.) Lonyangapuo, na sote hapa tumekuja kulizungumzia jambo hili akijua kwamba usalama unapokosekana Homa Bay unaweza kutatiza usalama wa Kenya nzima. Wataalamu wanasema kwamba insecurity anywhere is a threat to securityeverywhere . Kwamba, ukosefu wa usalama mahali pamoja, unaweza kuathiri mahali pengine. Kwa hayo mengi, ningependa kumwunga mkono ndugu yangu, Prof. Lonyangapuo, kwa kuleta Hoja hii ambayo itaimarisha hali yetu ya usalama kwa kuongeza idadi yetu ya polisi katika taifa letu la Kenya."
}